CAMEROON YAPATA USHINDI KWA TAABU
Nahodha wa Cameroon Samwel Eto’o
katika mechi ya kujipima nguvu ambayo The indomitable Lions iliishinda
Macedonia mabao 2-0 nchini Austria.
Mshambulizi huyo wa Chelsea hakuchezeshwa kutokana na jeraha la goti, huku Cameroon ikimpoteza mshambulizi mwingine Pierre Webo kutokana na jeraha siku ya Jumatatu punde baada ya kufunga.
Jean-Eric Maxim Choupo-Moting baadae akaongeza bao la pili.
Kipa Charles Itandje, mlinzi Jean-Armel Kana-Biyik na viungo Edgar Salli, Jean II Makoun na Stephane Mbia wote wanauguza majeraha tofauti.
Cameroon bado wana mechi za kujipima nguvu dhidi ya Paraguay, Ujerumani na Moldova kabla ya kombe la dunia.