SUAREZ: WAURUGUAY WAMTISHIA KIFO DUMMETT
Jeraha la Suarez sasa mashabiki wa Uruguay wamlaumu mlinzi wa Newcastle Paul Dummett.
Mlinzi wa Newcastle Paul Dummett ametishiwa
maisha yake na mashabiki wa Uruguay wanaomlaumu kwa kusababisha jeraha
lililomlazimu Luis Suarez kufanyiwa upasuaji ambao sasa wanahofu huenda
ikaathiri uwezo wake katika kombe la dunia .Dummett ametajwa katika kikosi cha Wales kinachopangiwa kuchuana na Uholanzi katika mechi ya kujipima nguvu juma lijalo.