DIEGO COSTA AENDA KWA SANGOMA WAKE
MSHAMBULIAJI Diego Costa amesafiri kwenda Belgrade kumuona mganga wa kienyeji Marijana Kovacevic maarufu kama 'Dokta Miujiza' kuhakikisha anakuwa fiti tayari kucheza mechi kubwa zaidi maishani mwake.
Mserbia huyo anatumia placenta kuwasaidia wachezaji kupona haraka matatizo ya misuli na Jumamosi Costa anataka kuichezea Atletico Madrid dhidi ya Real Madrid katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Costa anasumbuliwa na maumivu ya nyama, aliyoyapata katika mechi ya mwisho ya La Liga dhidi ya Barcelona, ambayo Atletico ilitoa sare ya 1-1 na kutwaa taji la Ligi hiyo Kuu Hispania.
Maumivu ya aina hiyo kwa kawaida yanawaweka wachezaji née ya Uwanja kwa siku zisizopungua 15, ambayo itamfanya aukose mchezo wa Lisbon iwapo tiba hiyo ya asili haitafanya kazi.
Costa ataungana tena na Atletico Madrid leo akitokea Serbia. Kovacevic amewatibu nyota kadhaa wa Ligi Kuu England halo kabla, akiwemo mshambuliaji Robin van Persie alipokuwa Arsenal na kiuno wa Chelsea, Frank Lampard.