JULIO AMTUNISHIA KIFUA KABURU, AMUAMBIA “TUNAOMBA PENZI KWA DEMU MMOJA, MWENYE BAHATI YAKE ATABEBA TOTOZ”

KOCHA wa Mwadui FC ya Shinyanga, Jamhuri Kihwelu 'Julio' amekifafananisha kitendo cha kuwania uongozi katika klabu ya Simba na maamuzi ya mwanaume kumtongoza mwanamke.

Akichukua fomu kwenye ofisi za makao makuu ya Simba mjini Dar es Salaam jana kuwania Umakamu wa Rais wa Simba katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo utakaofanyika Juni 29 mwaka huu, Julio amesema kuwania uongozi wa Simba kunafanana sana na kumtongoza mwanamke.
Nipeni mimi; Julio akiwahutubia wanachama wa Simba SC alipokwenda kuchukua fomu jana na chini ni mpinzani wake Kaburu

Julio atawania nafasi hiyo dhidi ya viongozi waliomaliza muda wao, Geoffrey Nyange
‘Kaburu’, Joseph Itang’are ‘Kinesi’ na Swedi Nkwabi- ambao walikuwa mabosi wake alipokuwa kocha wa timu hiyo.
"Nimeamua kuwania uongozi ndani ya klabu ya Simba kwa sababu nina haki ya kikatiba ya kugombea nafasi yoyote. Kugombea uongozi Simba ni sawa na kutongoza mwanamke kwani hata kama akikubali utapata sifa na akikataa unapata sifa vile vile," alisema Julio.
Kessy Kikoti naye alirejesha fomu 
Aidha, Julio, licha ya kuiongoza Mwadui FC kumaliza nafasi ya pili katika Kundi C la michuano ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu huu, amesema bado anatambua kuwa yeye ni kocha halali wa Simba kwa sababu "kikao kilichowafukuzisha kazi kilikuwa batili na ndiyo maana Shirikisho la Soka nchini (TFF) liliyakataa mapinduzi na kumrudisha mwenyekiti wao Ismail Aden Rage madarakani."

"Kwa watu wenye kuona mbali ninaamini watanipa kura Simba kwa sababu mimi ni kocha pekee niliyekuwa ninakubali kufundisha Simba bila kulipwa mshahara na sasa ninaudai uongozi wa Dalali Sh. milioni 24 na nilikubali kupoteza hadi gari langu kwa ajili ya Simba," amesema zaidi Julio ambaye baadaye alasiri amewahutubia kwa dakika chache wapenzi wa Simba waliojitokeza kumsindikiza kuchukua fomu.

Akiwa msaidizi wa aliyekuwa kocha mkuu wa Simba, Abdallah 'King' Kibadeni, Julio na nyota huyo wa zamani mwenye rekodi pekee ya kufunga magoli matatu pekee yake katika mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga, walitimuliwa baada ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu huu baada ya kuitishwa kwa kikao batili cha Kamati ya Utendaji ya Simba ambacho Rage hakuhudhuria.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA