Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2024

IHEFU SC SASA KUITWA SINGIDA LEOPARDS FC

Picha
Baada ya klabu ya Ihefu FC kuhamia Mkoani Singida rasmi ambapo watakua wakitumia Uwanja wa CCM Liti pale Singida Kwa mujibu wa Ripoti mbalimbali inasemekana kwamba Ihefu ipo kwenye mchakato wa kubadilisha jina lake na kuitwa Singida Leopard FC kuanzia Msimu unaokuja Wakati huo inasemekana kua Klabu ya Mbeya Kwanza FC ipo kwenye mchakato wa kununuliwa na itabadilishwa jina na kuitwa Ihefu FC Wakati huo huo Singida Fountain Gate itabadilishwa jina na kua Fountain Gate Academy na makao yake yatakuwa Mwanza kwenye Uwanja wa Fountain Gate uliopo Gwambina.

GAMONDI- MIMI SIO KOCHA WA KUZUIA KWA KUKABA

Picha
Gamondi “Mimi sio kocha ambaye napendelea kuzuia timu kwa kukaba dakika 90, mpira kwangu ni kama tamasha la maonesho nafikiri mkinifuatilia utagundua niliwahi kuja hapa zamani, soka langu ni la kushambulia na siwezi kubadilisha sanaa ya soka langu bila kujali nakutana na mpinzani wa namna gani nitaheshimu wapinzani wangu lakini kwangu heshima sio hofu” “Kila ninapoandaa timu naanda timu kushinda na si vinginevyo mimi ninawaamini wachezaji wangu kwa kiasi kikubwa nimewahi kucheza na Al Ahly nikiwa na Platnumz Stars na kuwa klabu ya kwanza kuifunga Al Ahly kutoka Afrika Kusini, Kwahiyo sina wasiwasi wala hofu ya kucheza dhidi ya timu kubwa” Miguel Gamondi

VLADMIR PETROVIC KOCHA MKUU ALGERIA

Picha
Shirikisho la Soka nchini Algeria [FAF] limemteua kocha Vladmir Petrovic mwenye umri wa Miaka (60) raia wa Bosnia and Herzegovina kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya Taifa hilo akichukua nafasi ya Kocha Djamel Belmadi aliyefutwa kazi mwezi Uliopita. Vladimir Petkovic atakuwa na kibarua cha kuisaidia timu hiyo kufuzu kwa michuano ya AFCON 2025 nchini Morocco na Kombe la Dunia la 2026 katika nchi za Mexico , Canada na Marekani, Kocha Huyo amewahi kuionoa timu ya Taifa ya Swirtzerland, na Klabu za Lazio ya Italia, Young Boys FC Sioni za Switzerland Pamoja na Bordeaux ya Ufaransa L

MO DEWJI ADAI AMEINUNUA SIMBA

Picha
Mohammed Dewji "Nafikiri kitu cha gharama zaidi nilichonunua kwenye maisha yangu ni klabu ya mpira ya Simba yenye zaidi ya mashabiki million 35 na niliipenda timu hii toka enzi za ujana wangu". *Niliinunua klabu hii miaka mitano iliyopita na nimeifanya klabu hii kuwa miongoni mwa klabu 10 bora zaidi barani Afrika ni jambo kubwa inaleta furaha sana". Mohammed Dewji, Mwekezaji wa Klabu ya Simba SC

INJINIA HERSI ASEMA YANGA HAIWEZI KUFIKA FAINALI YA LIGI YA MABINGWA

Picha
Rais wa klabu ya Yanga SC akiwa katika mahojiano na Televisheni ya Al Ahly amesema "binafsi naamini fainali ya CAF Champions League msimu huu ni baina ya Al Ahly dhidi ya Mamelodi Sundowns”, Al Ahly na Mamelodi ni timu zenye mikakati na ubora wa hali ya juu kwasasa Barani Afrika. Hersi aliendelea kusisitiza, “ikumbukwe Al Ahly ndio timu yenye uwekezaji mkubwa sana tena inapofika hatua za mtoano katika michuano hii, huku Mamelodi wakiwa ni mabingwa AFL na sidhani itakuwa rahisi kwao kuishia robo au nusu fainali.

MOHAMED CHUMA ALIKUWA BEKI WA KATI TAIFA STARS

Picha
MOHAMED Ali Chuma alikuwa ni mmoja wa mabeki wazuri kuwahi kutokea katika nchi hii ya Tanzania. Chuma alikuwa anamudu kucheza namba 3, 4, 5, na 6. Chuma alizaliwa katika kijiji cha Naumbu mkoani Mtwara 1943. Chuma alianza kung' ara katika michuano ya Sunlight Cup 1966 na baadaye katika Taifa Cup 1970/1973.  Chuma aling' ara pamoja na akina Sembwana Behewa, Mweri Simba, Abdallah Luo na Omary Zimbwe kutoka mkoani Tanga, akina Shiwa Lyambiko, Kasim Manga, Adam Sabu kutoka Morogoro. Chuma alikuwa na uwezo mkubwa wa kukaba winga au mshambuliaji hatari. Chuma katika timu ya Taifa Stars mwaka 1973 alicheza soka la hali ya juu na washambuliaji wengi wa Kenya kama akina Agonda Tukiyo au Allan Thigo walikuwa wanamuogopa na hata Timothy Aiyeko wa Uganda alikuwa anamhofia Chuma anapokutana nae. Chuma alikuwa ni mchezaji wa kiwango cha juu na ingekuwa miaka hii ya sasa Chuma angekuwa anaicheza soka barani Ulaya. Chuma miaka ya 1967 alikuwa anaichezea Beach Boys na akina Juma Gayo Mandoa, Mu...

SIMBA YAIJIBU YANGA, YAIPIGA TRA 6-0

Picha
Mabao matatu yaliyofungwa na kiungo mkabaji Sadio Kanoute na mengine ya Ladack Chasambi, Pah Omary Jobe na Freddie Michael Kobles yametosha kuiwezesha Simba SC kuifunga bila huruma TRA ya Kilimanjaro mabao 6-0 kwenye uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam. Mchezo huo wa kuwania kombe la Azam Sports Federation Cup, ASFA maarufu FA Cup, limeifanya Simba kutinga raundi ya 32 bora

PERCY TAU AWA MCHEZAJI GHALI AFRIKA

Picha
Vyanzo vikubwa vya habari Nchini Misri vimeripoti kuwa Kiungo Mshambuliaji wa Klabu ya Al Ahly,Percy Tau anatarajiwa kusaini Mkataba wa Miaka mitatu na Klabu hiyo ambapo atafanywa kuwa mchezaji anayelipwa zaidi ndani ya bara la Afrika. Mkataba mpya wa Tau katika klabu ya Al Ahly utamfanya kutia mfukoni Mshahara wa dola milioni 5.13 katika misimu mitatu ijayo ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 13 za Kitanzania.Mshahara ya kila mwaka akiwa na Klabu hiyo ilikuwa ni dola milioni 1.2 ikiwa ni zaidi ya Shilingi Bilioni 3 kwa Mwaka na sasa itaongezeka hadi dola milioni 1.3 (zaidi ya shilingi Bilioni 3.3 za Kitanzania) katika mwaka wa kwanza, dola milioni 1.4 (zaidi ya Shilingi Bilioni 3.7) kwa mwaka wa pili na dola milioni 1.6 (zaidi ya Shilingi Bilioni 4) kwa mwaka wa tatu. Kwenye Mkataba huo wa Tau inamaanisha Mwaka wa mwisho atakuwa anapokea Mshahara wa Shilingi Milioni 340 kwa Mwezi ambapo kwa wiki atakuwa anaramba Milioni 85,Milioni 12 kwa siku.

MAYELE AOMBA KUVUNJA MKATABA PYRAMIDS

Picha
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Yanga, Fiston Mayele amewasilisha barua kwenye Menejiment ya klabu ya Pyramids kwaajili ya kuhitaji kusitishiwa mkataba wake. Vyombo mbalimbali vya Habari kutoka Misri vimeripoti kuwa Fiston Mayele hana furaha kuitumikia zaidi Pyramids na ameshafanya mazungumzo na Menejiment yake ili kupata changamoto nyingine akiondoa Pyramids. Taarifa za kuaminika ni kuwa Fiston Mayele anautaka usimamizi wa klabu ya Pyramids ya nchini Misri kuweza kusitisha mkataba wake, Fiston Mayele needs the pyramids management to terminate his contract and leave the club.

RIGOBERT SONG ATIMULIWA CAMEROON

Picha
Kocha Rigobert Song hatoendelea kuwa kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Cameroon Kocha huyo mwenye umri wa Miaka (47) amemaliza mkataba wake na Shirikisho la soka la nchi hiyo FECATOOT limeamua kuachana nae. Takwimu za Rigobert Song Akiwa na Timu ya Taifa ya Cameroon. 🏟 Mechi: 23 ✅ Kushinda: 5 🤝 Sare: 9 ❌ Kupoteza: 9

REKODI ZA MAYELE MAJANGA

Picha
Fiston Mayele katika CAF CHAMPIONS LEAGUE msimu huu. Mechi: 4️ Magoli: 0️ Assist: 1️ Shots on Target: 6️ Shots of Target: 4️ Big Chance Missed: 5️ Big Chance Created: 0️ Nikisema kuwa Mayele alibebwa na ubora wa kikosi cha Yanga nitakuwa nimekosea wakuu. Mayele

DAKTARI WA AZAM FC AFARIKI DUNIA

Picha
Klabu ya Azam FC, imetangaza kifo cha aliyekuwa daktari wa timu hiyo, Mwanandi Mwankemwa, kilichotokea leo jioni katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke. Dkt. Mwankemwa alianza majukumu yake Azam FC, mwaka 2008, na katika kipindi chote cha utendaji wake, amehusika kuwasindikiza wachezaji katika matibabu ya ndani na nje ya nchi. Mwankemwa aliingia katika udaktari michezoni mwaka 1982 na wakati huo alianza na timu JKT Ruvu, Sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake yeye sote tutarejea Dk Mwamkemwa

YANGA IMENIPA HESHIMA- PACOME

Picha
" Ni kweli niliumia siku moja kabla ya mchezo dhidi ya CR Belouizdad ulikua wakati mgumu sana kwangu nakumbuka wachezaji wenzangu wote walikua tayari kwa mchezo" "Ilivyofika asubuhi niliufuata uongozi wa Yanga pamoja na kocha nikamwambia sidhani kama ni sahihi kwangu kukaa kwa kubweteka nimeona ni kwa namna gani mashabiki wamejiandaa kwaajili ya hii siku yangu iweje leo hii na mimi nishindwe kufanya jambo kwaajili yao? "Namshkuru Mungu alikua upande wangu na Yanga kwa ujumla tukafanikiwa kuifunga Cr Belouzidad goli 4 ambazo zilituvusha moja kwa moja" "Pengine najivunia kuingia katika historia hii kubwa ya klabu kubwa kama @yangasc kuwa miongoni mwa wachezaji walioisaidia timu yao kutinga hatua ya makundi baada ya miaka 25 pamoja na kutinga hatua ya robo fainali kwa mara ya Kwanza" "Tunaelekea misri tukiwa tunauhitaji sana mchezo pamoja na nafasi ya kwanza wananchi waongeze Dua kwasababu ni watu wenye upendo sana na wachezaji wao naimani itatusaid...

MOSES PHIRI AANZA KUTUPIA ZAMBIA

Picha
Mshambuliaji hatari,Mosses Phiri hapo jana (Jumapili) aliifungia bao timu yake ya Power Dynamos na kufanikisha kupata alama moja dhidi ya wababe Zesco United. Hii ni mechi ya kwanza kwa Phiri tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Simba Sc

YANGA KUELEKEA CAIRO LEO

Picha
Na Van Mapande Jr Klabu ya Young Africans SC itaanza Safari yake leo majira ya 11:55 jioni kuelekea Cairo Misri Msafara wake utakuwa wa watu (60) Utajumuisha wachezaji (24), Benchi la Ufundi Lenye watu (13) na viongozi pamoja na mashabiki (23) Yanga Itashuka Dimbani Siku ya Ijumaa majira ya saa moja kamili usiku kwa masaa ya Afrika mashariki watamenyana na Al Ahly kukamilisha mchezo wa hatua ya Makundi, Yanga anahitaji alama tatu ili afanikiwe kuongoza kundi lake.

AKINA MKOJANI WAMETURUDISHIA LADHA ZA BONGO MUVI

Picha
Na Prince Hoza BINAFSI mimi tangu walipoondoka kwenye tasnia ya maigizo hapa nchini nyota kama Steven Kanumba, Mzee Majuto, Sharo Milionea na Mzee Small niliona tasnia hiyo imeondokewa na watu muhimu sana.  Kiwanda cha bongomuvi kama kinavyojulikana kwasasa nimekiona kama kimekaukiwa, wasanii waliobaki nimewaona kama wachanga na wameshindwa kuiweka kwenye matawi ya juu, nikianzia kwa Kanumba, yeye pekee aliisaidia bongomuvi kujitangaza nje ya mipaka yetu.  Kanumba aliifanya Tanzania kujulikana na kuwafanya wasanii wetu kupiga hatua, wasanii wakubwa wa Nigeria haikuwa.  Bongomuvi ilikosa ubunifu na ikajikuta kuwa kundi la umbea na kusemana vibaya wao kwa wao na kuleta tafrani, Kanumba alifariki dunia ingawa kazi zake bado ziliendelea kuitangaza Tanzania kimataifa, sawa na kazi za Mzee Majuto na Small Wangamba ambao nao walikuwa kivutio kwenye tasnia hiyo. Wasanii hao waliaga dunia, bado mchango wao ni mkubwa sana, wakati mastaa hao wakifariki, kijana mwingine Sharo Milionea naye alikuja...

HARMONIZE KUSAINI WAPYA WAWILI KONDE GANG

Picha
Boss wa lebo ya Konde Gang, #Harmonize ametangaza kusaini wasanii wapya wawili mwaka huu 2024 kwenye lebo hiyo na kuongeza kuwa isingekuwa ushauri wa msanii wake Ibraah basi angekata tamaa kusapoti wasanii wengine. KondeGang hivi sasa imebaki na msanii mmoja pekee ambaye ni Ibraah baada ya wasanii wengine akiwemo Country Wizzy, Killy, Cheed na Anjella kuondoka katika nyakati tofauti. Harmonize

KENNEDY MUSONDA: STRAIKA ANAYETUMIKA KAMA WINGA

Picha
NI mshambuliaji mwenye matumizi mazuri ya nafasi anazopata na mtekelezaji Mzuri wa majukumu anayopewa. Mda mwingi kocha anamtumia kama winga wa kulia,Nafikiri kasi yake imemfanya Mwalimu kumtumia kwenye eneo Hilo au ule uwezo wake wa kujenga shambulizi kwa kasi kubwa au vyote kwa pamoja Mwalimu kaviona. unapomtumia kama mshambuliaji namba mbili yaani 10 kasi yake na control yake inalazimisha sana beki kuchoka haraka mno na nihatari kwa timu pinzani akitokea Sub kwani ni ngumu sana mlinzi kumdhibiti kirahisi kwasababu yeye anaingia na kasi yake wakati mlinzi kachoka. Anapopewa jukumu la namba 9 Musond anapenda kucheza Tisa kimvuli akizunguka eneo zima la ushambuliaji na malanyingi anaongeza nguvu kwenye viungo washambuliaji ndiyo maana ni nadra sana kumkuta kwenye mtego wa kuotea. Kennedy Musonda .

YAMMI HAJAWAHI KUWA NA MPENZI

Picha
Mwimbaji wa Bongofleva kutoka The African Princess Label, Yammi amesema katika maisha yake hajawahi kuwa na mpenzi!. "Sina mwanaume, bado, sijawahi kuwa naye (mpenzi), sijawahi kuwa katika mahusiano kabisa," amesema Yammi. Princess Yammi hajawahi kuwa na mpenzi

INONGA MGENI RASMI SIMBA VS JWANENG

Picha
“Mgeni rasmi katika mchezo dhidi ya Jwaneng Galaxy ni Henock Inonga sababu ndio mchezaji pekee katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ameifikisha timu yake ya taifa DR Congo kwenye nafasi ya nne kwenye AFCON iliyomalizika hivi karibuni. Hayo yamesemwa na Afisa Habari wa klabu ya Simba, Ahmed Ally, tayari wachezaji wa Simba wamewasili leo wakitokea Ivory Coast ambapo walienda kucheza na Asec Mimosas na kutoka sare tasa 0-0 Inonga

JWANENG GALAXY KAJA MDA MBAYA- AHMED ALLY

Picha
“Huu sio muda wa kufanya kingine chochote, huu ni muda wa kujipanga kwenda kumuua Jwaneng Galaxy. Tufanye maandalizi ya maana kwenye matawi yetu na kujipanga kila mtu ajipange Simba tupo wengi nchi hii. Tutambue tunaelekea kwenye vita ya kisasi, Mwanasimba anayenunua tiketi ajue kwamba hajanunua tiketi tu, amenunua silaha ya kisasi. Twende tukatinge robo fainali.” “Kama kawaida kutakuwa na hamasa, na sisi ndio wataalamu wa hamasa. Wiki iliyopita nimeona hamasa za kitoto. Wiki hii tutafanya hamasa kubwa mno na tutafanya kwa ubora. Jumatano tutafanya uzinduzi wa hamasa katika tawi la Tunawakera lililopo Keko Maduka Mawili kuanzia saa 3 asubuhi. Msafara utaanzia Keko Furniture.” “Tarehe 29 tutafanya hamasa ndani ya mabasi ya mwendokasi kuanzia saa 3 asubuhi katika kituo cha mwendokasi Gerezani muhimu uvae jezi yako ya Simba. Kutakuwa na mabasi maalumu ambayo tutazunguka mjini hapa kupiga kampeni. Hii sio mara ya kwanza kufanya kampeni kwa kutumia chombo cha moto, tulishawahi kufanya kweny...

FEITOTO AZIDI KUTISHA KWA MABAO LIGI KUU BARA

Picha
Kiungo wa Klabu ya Azam Feisal Salum amezidi kuweka rekodi kubwa ndani ya Ligi Kuu Tanzania bara mara baada ya hapo Jana kufikisha magoli Tisa ndani ya Ligi hiyo ambapo Azam ilicheza dhidi ya Tanzania Prison na mchezo kumalizika Kwa sare ya 1-1. Kufikisha idadi hiyo ya magoli kunamfanya kuendelea kuwa Mchezaji kjnara ndani ya Klabu ya Azam ambayo imefunga magoli 39 kwenye Michezo 17 ya Ligi huku akimkaribia kinara wa Ligi Kuu Tanzania Aziz Ki mwenye magoli 10 mpaka sasa. Toka Feisal ajiunge na Ligi Kuu Tanzania Mwaka 2018 akiwa na Klabu ya Yanga hajawahi kuwa na rekodi Bora ya kufunga kama msimu huu kwani mara kadhaa aliisbia kufunga magoli Sita. Hii ni dalili kuwa Kiungo huyo amejitosa mazima kwenye mbio za kuwania kiatu cha Mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania bara 2023/24. Feitoto

RAIS SAMIA AIPONGEZA YANGA KUTINGA ROBO FAINALI

Picha
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, ameipongeza Yanga SC, kwa kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kuishushia kichapo cha mabao 4-0 CR Belouizadad jana Jumamosi. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rais Samia ameandika “Naipongeza Klabu ya Yanga kwa kufanya vyema katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), na kufanikiwa kufuzu hatua ya Robo Fainali. Mafanikio haya yameandika historia kubwa kwa klabu na sekta ya michezo nchini. Mmeleta furaha kwa mamilioni ya mashabiki wenu na Watanzania kwa ujumla.

SIMBA WAANZA SAFARI YA TANZANIA

Picha
Kikosi cha Simba kimeanza safari ya kurejea Nchini Tanzania kikitokea Ivory Coast tayari kwa maandalizi ya mchezo wa kufa na kupona dhidi ya Jwaneng Galaxy ambapo Simba inatakiwa kushinda ili iungane na Yanga kwenye hatua ya Robo Fainali ya Klabu Bingwa Barani Afrika.

SIMBA SASA KUSAJILI MSHAMBULIAJI MWINGINE

Picha
Tetesi zinaeleza kuwa viongozi wa Simba SC wanapanga kufanya jaribio la kumsajili mshambuliaji wa Al Ittihad Alexandria Club ya nchini Misri, Agostinho Cristóvão Paciência maarufu kama Mabululu. Jaribio hilo linatarajiwa kufanyika dirisha kubwa la usajili mwaka huu Kwa ajili ya kuboresha safu ya ushambuliaji ya timu hiyo na kuhakikisha wanakuwa imara sana. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 31 ni moja kati ya wachezaji walioisaidia timu ya taifa ya Angola 'swala weusi' kufanya vyema kwenye michuano ya AFCON iliyofanyika mwanzoni mwaka huu pale Ivory Coast.

IHEFU SC YAHAMIA SINGIDA

Picha
Ihefu SC imehamia mkoani Singida hii ni baada ya kuuchagua uwanja wa CCM Liti kama uwanja wao wa nyumbani kwa msimu mzima. Leo watendaji wote wa timu za ligi kuu wametumiwa taarifa rasmi ya kuwa michezo yote ya nyumbani ya Ihefu SC itachezwa CCM Liti, Singida, Taarifa ya Bodi imesema kuwa Ihefu SC itatumia uwanja wa CCM Liti Singida badala ya HIGHLAND ESTATE, Ubaruku, Mbeya. Wakati huohuo, Singida Fountain Gate FC imeuchagua uwanja wa CCM Kirumba kama uwanja wao wa nyumbani mpaka mwishoni mwa msimu huu.

ZUCHU AVUNJA REKODI

Picha
Malkia wa bongofleva nchini Zuchu amevunja rekodi baada ya kufikisha watazamaji zaidi ya 500 milioni katika mtandao wa youtube. Zuchu ndiye msanii wa kike wa kwanza kufikisha total views zaidi ya 500 milioni katika mtandao wa YouTube East Africa.  Hivi ni yeye malkia wa muziki East Africa? Zuchu

TSHISEKEDI KUMZAWADIA MCHEZAJI WA RAYON SPORTS

Picha
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi ametangaza kumpatia zawadi mchezaji Luvumbu Nzinga ambaye ameachana na klabu ya Rayon Sports ya Rwanda hivi karibuni. Katika mkutano na waandishi wa habari alifahamisha kuwa Luvubu alionyesha ushujaa katika kuwapigania wananchi wa DRC waliopo Kaskazini mwa nchini hiyo ambao wanaendelea kuyakimbia makazi yao kutokana na mapigano yanayowahusisha jeshi la nchi na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda. Pia aliweka wazi kuzungumza na Mwenyekiti wa timu ya AS Vita Club na kukubali kumsaini mchezaji huyo baada ya kuachana na Rayon Sports. Luvumbu Hivi karibuni ushangiliaji wake ulizua mjadala nchini Rwanda na kupelekea Shirikisho la soka Rwanda FERWAFA, kumsimamisha miezi sita kujihusisha na soka kwa madai ya kuchanganya soka na siasa.

ALI KAMWE AZIMIA KWA MKAPA

Picha
WAKATI mashabiki wa Yanga wakishangilia ushindi wao baada ya kuichapa CR Belouizdad mabao 4-0 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi, hali imekuwa sio nzuri kwa ofisa habari na mawasiliano wa klabu hiyo, Ally Kamwe baada ya kuzimia. Kamwe amekumbana na hali hiyo wakati akishangilia ushindi huo kwenye vyumba vya kubadilishia nguo akajikuta anaanguka na kupoteza fahamu. Baada ya tukio hilo, Kamwe akachukuliwa na kutolewa nje ya uwanja kisha kuwahishwa hospitalini baada ya kupatiwa matibabu akiwa ndani ya gari la wagonjwa. Katibu wa Madaktari wa Tiba za Wanamichezo nchini Dr Juma Sufian amethibitisha tukio hilo huku akiomba apewe muda kwani yuko kwenye harakati za kumsaidia msemaji huyo. "Ni kweli huyu ni Kamwe amepatwa na tatizo la kupoteza fahamu, tupeni muda tumsaidie haraka ili arejee kwenye afya yake,"amesema Sufian ambaye ni daktari wa zamani wa Yanga. Ali Kamwe

YANGA YATINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA

Picha
Wawakilishi wa Tanzania katika michuaño ya Ligi ya mabingwa Afrika, Yanga SC usiku huu imetinga robo fainali baada ya kuilaza CR Belouizdad ya Algeria mabao 4-0 katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam. Haikuwa rahisi Yanga kushinda mabao hayo manne kwani iliwahi kufungwa 3-0 hivyo ilitakiwa kushinda nne ili isonge mbele. Mabao ya Yanga yalifungwa na Mudathir Yahya dakika ya 42, Stephanie Aziz Ki dakika ya 46, Kennedy Musonda dakika ya 48 na Joseph Guede dakika ya 84, Yanga sasa itaenda Misri kucheza na Al Ahly mchezo was kukamilisha ratiba

MHE MWIGULU KAMA PACOME

Picha
Muonekano mpya wa mhe Dkt Mwigulu Nchemba ambaye ni Waziri wa fedha, kuelekea mtanange wa kukata na shoka kati ya Yanga SC ya Tanzania na CR Belouizdad ya Algeria utakaofanyika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, Waziri Nchemba amepiga briech akijifananisha na Pacome Zouzoua. Wachezaji wa Yanga karibu wote wamepiga briech wakiadhimisha siku ya kuzaliwa ya Pacome Dkt Mwigulu, kama Pacome

RICH MAVOKO AREJEA KWA KISHINDO KWENYE BONGOFLEVA

Picha
Baada ya Rich Mavoko kurejea rasmi kwenye muziki kwa wimbo wake 'miss you ' hadi sasa chini ya masaa 15 video ya wimbo huo ina jumla views 60k YouTube. Ndo mwanzo ameanza baada ya kunyamaza kwa muda. Labda tutarajie kurudi kuendeleza alipoachia!!! Jambo litakalo ufanya muziki wake ukose kwenda juu kwa kasi ni marufuku kuonekana kwenye media.

YANGA WAKISHINDA 4-0 WANAFUZU MOJA KWA MOJA

Picha
Yanga wanahitaji kushinda 4 dhidi ya CR Belouzdad ili kufuzu moja kwa moja leo Wakishinda hizo wametinga robo fainali bila kusubiri mechi ya Ahly. Wakishinda chini ya hapo watatakiwa kwenda kutafuta alama 1 kule Cairo kwa Ahly! Wakisare watatakiwa kwenda kushinda kule kwa Ahly kisha waombe Belouzdad atoe sare dhidi ya Medeama au apoteze

SIMBA YANUKIA ROBO FAINALI

Picha
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC usiku huu imeilazimisha Asec Mimosas sare tasa 0-0 katika uwanja wa Humphrey Felix mjini Abidjan nchini Ivory Coast na kushika nafasi ya pili nyuma ya Asec iliyofuzu robo fainali ya Ligi ya mabingwa Afrika. Simba sasa inasubiri mchezo wake wa mwisho dhidi ya Jwaneng Galaxy utakaofanyika jijini Dar es Salaam. MSIMAMO WA KUNDI B 1. Asec (5) — 11pts 2. Simba (5) — 6pts 3. Jwaneng (4) — 4pts 4. Wydad (4) — 3pts

ZALAN FC YAWEKA REKODI SUDAN KUSINI

Picha
Zalan FC imekuwa timu ya kwanza ya Sudan Kusini kushinda Ligi Kuu na Super Cup kwa mkupuo tangu kuasisiwa kwa Taifa hilo. Hayo ni mafanikio makubwa kwa klabu hiyo maarufu kama Kazuk ama wakali wa Rumbek ambao wamejipambanua vyema kwa nia yao ya dhati na uthubutu mkubwa kulibeba soka la Sudani Kusini Kimataifa. Kazuk Warriors imekiri mafanikio hayo ni ya kujivunia zaidi kwa kipindi hiki na wanatarajia kuyafurahia kwa majuma kadhaa!

CR BELOUIZDAD WAKIFANYA MAZOEZI YAO UWANJA WA MKAPA

Picha
Kikosi cha CR Belouzidad kimefanya mazoezi yake ya mwisho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jioni ya leo kabla ya kuwavaa Yanga SC hapo kesho.