MOHAMED CHUMA ALIKUWA BEKI WA KATI TAIFA STARS
MOHAMED Ali Chuma alikuwa ni mmoja wa mabeki wazuri kuwahi kutokea katika nchi hii ya Tanzania. Chuma alikuwa anamudu kucheza namba 3, 4, 5, na 6.
Chuma alizaliwa katika kijiji cha Naumbu mkoani Mtwara 1943. Chuma alianza kung' ara katika michuano ya Sunlight Cup 1966 na baadaye katika Taifa Cup 1970/1973.
Chuma aling' ara pamoja na akina Sembwana Behewa, Mweri Simba, Abdallah Luo na Omary Zimbwe kutoka mkoani Tanga, akina Shiwa Lyambiko, Kasim Manga, Adam Sabu kutoka Morogoro.
Chuma alikuwa na uwezo mkubwa wa kukaba winga au mshambuliaji hatari.
Chuma katika timu ya Taifa Stars mwaka 1973 alicheza soka la hali ya juu na washambuliaji wengi wa Kenya kama akina Agonda Tukiyo au Allan Thigo walikuwa wanamuogopa na hata Timothy Aiyeko wa Uganda alikuwa anamhofia Chuma anapokutana nae.
Chuma alikuwa ni mchezaji wa kiwango cha juu na ingekuwa miaka hii ya sasa Chuma angekuwa anaicheza soka barani Ulaya. Chuma miaka ya 1967 alikuwa anaichezea Beach Boys na akina Juma Gayo Mandoa, Musa Okelo, Issa Pele, Muhaji Mukhi na wengineo.
Chuma alikuwa anang' a sana anapokuwa na klabu yake ya Nyota FC ya Mtwara akicheza na akina Abdurahman Zimbo, Iddi Pazi, Ibrahim Shomar, Iddi Dogoa na Bakari Bomba.
Wengine ni Denis Mrope, Isaya Namajojo, Mohamed Mkandinga, Said nyingema, Rashid Hanzuruni, Juma Kibonge, Amin Buljji, Mzee Kwasa, Joseph Agostino na Hamisi Masika.
Chuma pia katika timu ya mkoa wa Mtwara katika kombe la Taifa, Taifa Cup alicheza na akina Haji Masoud, Hamim Mawazo, Shomar Seleman, Juma Mkambi "General" na Seleman Omary.
Chuma 1974 alikuwepo katika timu iliyochukua kombe la Chalenji akiwa na akina Omary Mahohamed, Chuma alikuwepo katika timu ya taifa, Taifa Stars 1973 iliyoshiriki mechi za kufuzu za AFKON akiwa na kocha Shabani Marijani.
Na nyota wangine akina Sunday Manara, Willy Mwaijibe, Jumanne Hassan, Haidar Abeid, Abdallah Kibaden, Mustafa Kasimu, Shabani Baraza, Omary Zimbwe, Mwabuda Mwihaji na Nassoro Mashoto, Chuma alistaafu rasmi kucheza soka