YANGA YATINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA
Wawakilishi wa Tanzania katika michuaño ya Ligi ya mabingwa Afrika, Yanga SC usiku huu imetinga robo fainali baada ya kuilaza CR Belouizdad ya Algeria mabao 4-0 katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
Haikuwa rahisi Yanga kushinda mabao hayo manne kwani iliwahi kufungwa 3-0 hivyo ilitakiwa kushinda nne ili isonge mbele.
Mabao ya Yanga yalifungwa na Mudathir Yahya dakika ya 42, Stephanie Aziz Ki dakika ya 46, Kennedy Musonda dakika ya 48 na Joseph Guede dakika ya 84, Yanga sasa itaenda Misri kucheza na Al Ahly mchezo was kukamilisha ratiba