DAKTARI WA AZAM FC AFARIKI DUNIA
Klabu ya Azam FC, imetangaza kifo cha aliyekuwa daktari wa timu hiyo, Mwanandi Mwankemwa, kilichotokea leo jioni katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke.
Dkt. Mwankemwa alianza majukumu yake Azam FC, mwaka 2008, na katika kipindi chote cha utendaji wake, amehusika kuwasindikiza wachezaji katika matibabu ya ndani na nje ya nchi.
Mwankemwa aliingia katika udaktari michezoni mwaka 1982 na wakati huo alianza na timu JKT Ruvu, Sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake yeye sote tutarejea