HARMONIZE KUSAINI WAPYA WAWILI KONDE GANG
Boss wa lebo ya Konde Gang, #Harmonize ametangaza kusaini wasanii wapya wawili mwaka huu 2024 kwenye lebo hiyo na kuongeza kuwa isingekuwa ushauri wa msanii wake Ibraah basi angekata tamaa kusapoti wasanii wengine.
KondeGang hivi sasa imebaki na msanii mmoja pekee ambaye ni Ibraah baada ya wasanii wengine akiwemo Country Wizzy, Killy, Cheed na Anjella kuondoka katika nyakati tofauti.