ZALAN FC YAWEKA REKODI SUDAN KUSINI
Zalan FC imekuwa timu ya kwanza ya Sudan Kusini kushinda Ligi Kuu na Super Cup kwa mkupuo tangu kuasisiwa kwa Taifa hilo.
Hayo ni mafanikio makubwa kwa klabu hiyo maarufu kama Kazuk ama wakali wa Rumbek ambao wamejipambanua vyema kwa nia yao ya dhati na uthubutu mkubwa kulibeba soka la Sudani Kusini Kimataifa.
Kazuk Warriors imekiri mafanikio hayo ni ya kujivunia zaidi kwa kipindi hiki na wanatarajia kuyafurahia kwa majuma kadhaa!