YANGA KUELEKEA CAIRO LEO
Na Van Mapande Jr
Klabu ya Young Africans SC itaanza Safari yake leo majira ya 11:55 jioni kuelekea Cairo Misri Msafara wake utakuwa wa watu (60) Utajumuisha wachezaji (24), Benchi la Ufundi Lenye watu (13) na viongozi pamoja na mashabiki (23)
Yanga Itashuka Dimbani Siku ya Ijumaa majira ya saa moja kamili usiku kwa masaa ya Afrika mashariki watamenyana na Al Ahly kukamilisha mchezo wa hatua ya Makundi, Yanga anahitaji alama tatu ili afanikiwe kuongoza kundi lake.