SIMBA SASA KUSAJILI MSHAMBULIAJI MWINGINE
Tetesi zinaeleza kuwa viongozi wa Simba SC wanapanga kufanya jaribio la kumsajili mshambuliaji wa Al Ittihad Alexandria Club ya nchini Misri, Agostinho Cristóvão Paciência maarufu kama Mabululu.
Jaribio hilo linatarajiwa kufanyika dirisha kubwa la usajili mwaka huu Kwa ajili ya kuboresha safu ya ushambuliaji ya timu hiyo na kuhakikisha wanakuwa imara sana.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 31 ni moja kati ya wachezaji walioisaidia timu ya taifa ya Angola 'swala weusi' kufanya vyema kwenye michuano ya AFCON iliyofanyika mwanzoni mwaka huu pale Ivory Coast.