INJINIA HERSI ASEMA YANGA HAIWEZI KUFIKA FAINALI YA LIGI YA MABINGWA
Rais wa klabu ya Yanga SC akiwa katika mahojiano na Televisheni ya Al Ahly amesema "binafsi naamini fainali ya CAF Champions League msimu huu ni baina ya Al Ahly dhidi ya Mamelodi Sundowns”, Al Ahly na Mamelodi ni timu zenye mikakati na ubora wa hali ya juu kwasasa Barani Afrika.
Hersi aliendelea kusisitiza, “ikumbukwe Al Ahly ndio timu yenye uwekezaji mkubwa sana tena inapofika hatua za mtoano katika michuano hii, huku Mamelodi wakiwa ni mabingwa AFL na sidhani itakuwa rahisi kwao kuishia robo au nusu fainali.