FEITOTO AZIDI KUTISHA KWA MABAO LIGI KUU BARA
Kiungo wa Klabu ya Azam Feisal Salum amezidi kuweka rekodi kubwa ndani ya Ligi Kuu Tanzania bara mara baada ya hapo Jana kufikisha magoli Tisa ndani ya Ligi hiyo ambapo Azam ilicheza dhidi ya Tanzania Prison na mchezo kumalizika Kwa sare ya 1-1.
Kufikisha idadi hiyo ya magoli kunamfanya kuendelea kuwa Mchezaji kjnara ndani ya Klabu ya Azam ambayo imefunga magoli 39 kwenye Michezo 17 ya Ligi huku akimkaribia kinara wa Ligi Kuu Tanzania Aziz Ki mwenye magoli 10 mpaka sasa.
Toka Feisal ajiunge na Ligi Kuu Tanzania Mwaka 2018 akiwa na Klabu ya Yanga hajawahi kuwa na rekodi Bora ya kufunga kama msimu huu kwani mara kadhaa aliisbia kufunga magoli Sita. Hii ni dalili kuwa Kiungo huyo amejitosa mazima kwenye mbio za kuwania kiatu cha Mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania bara 2023/24.