YANGA IMENIPA HESHIMA- PACOME
" Ni kweli niliumia siku moja kabla ya mchezo dhidi ya CR Belouizdad ulikua wakati mgumu sana kwangu nakumbuka wachezaji wenzangu wote walikua tayari kwa mchezo"
"Ilivyofika asubuhi niliufuata uongozi wa Yanga pamoja na kocha nikamwambia sidhani kama ni sahihi kwangu kukaa kwa kubweteka nimeona ni kwa namna gani mashabiki wamejiandaa kwaajili ya hii siku yangu iweje leo hii na mimi nishindwe kufanya jambo kwaajili yao?
"Namshkuru Mungu alikua upande wangu na Yanga kwa ujumla tukafanikiwa kuifunga Cr Belouzidad goli 4 ambazo zilituvusha moja kwa moja"
"Pengine najivunia kuingia katika historia hii kubwa ya klabu kubwa kama @yangasc kuwa miongoni mwa wachezaji walioisaidia timu yao kutinga hatua ya makundi baada ya miaka 25 pamoja na kutinga hatua ya robo fainali kwa mara ya Kwanza"
"Tunaelekea misri tukiwa tunauhitaji sana mchezo pamoja na nafasi ya kwanza wananchi waongeze Dua kwasababu ni watu wenye upendo sana na wachezaji wao naimani itatusaidia sana "