JWANENG GALAXY KAJA MDA MBAYA- AHMED ALLY
“Huu sio muda wa kufanya kingine chochote, huu ni muda wa kujipanga kwenda kumuua Jwaneng Galaxy. Tufanye maandalizi ya maana kwenye matawi yetu na kujipanga kila mtu ajipange Simba tupo wengi nchi hii. Tutambue tunaelekea kwenye vita ya kisasi, Mwanasimba anayenunua tiketi ajue kwamba hajanunua tiketi tu, amenunua silaha ya kisasi. Twende tukatinge robo fainali.”
“Kama kawaida kutakuwa na hamasa, na sisi ndio wataalamu wa hamasa. Wiki iliyopita nimeona hamasa za kitoto. Wiki hii tutafanya hamasa kubwa mno na tutafanya kwa ubora.
Jumatano tutafanya uzinduzi wa hamasa katika tawi la Tunawakera lililopo Keko Maduka Mawili kuanzia saa 3 asubuhi. Msafara utaanzia Keko Furniture.”
“Tarehe 29 tutafanya hamasa ndani ya mabasi ya mwendokasi kuanzia saa 3 asubuhi katika kituo cha mwendokasi Gerezani muhimu uvae jezi yako ya Simba.
Kutakuwa na mabasi maalumu ambayo tutazunguka mjini hapa kupiga kampeni. Hii sio mara ya kwanza kufanya kampeni kwa kutumia chombo cha moto, tulishawahi kufanya kwenye treni, tumewahi kufanya pia kwenye pantoni na muda huu ni ndani ya mwendokasi.”
“Tulichobakiza kufanya ni hamasa kwenye ndege na sababu Air Tanzania ni wadhamini wetu ipo siku tutakodi ndege kwenda Dodoma tukifanya kampeni.”
“Tukiwa kwenye hamasa wadau wetu CRDB Bank na NMB watakuwepo pia kuwafungulia akaunti mashabiki wetu.
“Sisi hatuwaogopi Jwaneng Galaxy, uoga ni kwa mtu dhaifu lakini la muhimu ni tahadhari kwa 100% ili yasije tokea ya mwaka 2021.”- Ahmed Ally.