AKINA MKOJANI WAMETURUDISHIA LADHA ZA BONGO MUVI

Na Prince Hoza

BINAFSI mimi tangu walipoondoka kwenye tasnia ya maigizo hapa nchini nyota kama Steven Kanumba, Mzee Majuto, Sharo Milionea na Mzee Small niliona tasnia hiyo imeondokewa na watu muhimu sana. 

Kiwanda cha bongomuvi kama kinavyojulikana kwasasa nimekiona kama kimekaukiwa, wasanii waliobaki nimewaona kama wachanga na wameshindwa kuiweka kwenye matawi ya juu, nikianzia kwa Kanumba, yeye pekee aliisaidia bongomuvi kujitangaza nje ya mipaka yetu. 

Kanumba aliifanya Tanzania kujulikana na kuwafanya wasanii wetu kupiga hatua, wasanii wakubwa wa Nigeria haikuwa. 

Bongomuvi ilikosa ubunifu na ikajikuta kuwa kundi la umbea na kusemana vibaya wao kwa wao na kuleta tafrani, Kanumba alifariki dunia ingawa kazi zake bado ziliendelea kuitangaza Tanzania kimataifa, sawa na kazi za Mzee Majuto na Small Wangamba ambao nao walikuwa kivutio kwenye tasnia hiyo.


Wasanii hao waliaga dunia, bado mchango wao ni mkubwa sana, wakati mastaa hao wakifariki, kijana mwingine Sharo Milionea naye alikuja na aidia yake ambayo ilimtambulisha vilivyo, Sharo alikuwa muigizaji wa kwanza kukubalika na kuwavutia wawekezaji. 

Makampuni mbalimbali yalijitokeza kumdhamini na kuingia naye  mikataba, kifo chake kilisononesha wengi kwani ndio kwanza alichipukia kwenye sanaa hiyo.

Kufariki kwa Kanumba, Mzee Majuto, Sharo Milionea na Mzee Small kuliifanya bongomuvi kulemaa na wengi waliacha kutazama muvi za kibongo na kukimbilia muvi za nje. 

Hata mimi niliacha kabisa kununua muvi za nyumbani na kujikuta natazama muvi za Kihindi, Kikorea, Kijapan, Kituruki na kwingine, muvi hizo zinatafsiliwa na madj wetu wa kibongo kama Dj Murph, Dj Maki na wengineo. 

Chumvi Nyingi

Sio siri muvi za nje zinavutia, licha kwamba wasanii wa Tanzania walishindana kutoa muvi zao lakini walizidiwa ubunifu.

Malalamiko ya hapa na pale kuhusu wasanii wetu kutaka muvi za nje ziondolewe kwenye soko, lakini wengi waligoma wakidai kwamba muvi za Tanzania zimekosa ubunifu hivyo wengi walikimbilia huko.

Mimi binafsi niliwahi kuwaponda bongomuvi na nikawataka wawe wabunifu ili kazi zao ziweze kushindana na muvi na nje zinazotafsiliwa na madj wetu. 

Kadri siku zinavyozidi kusonga mbele na wasanii wetu wanabadilika na kuongeza maarifa, wasanii kama Mkojani, Tin White na Chumvi Nyingi ni miongoni mwa wasanii wanaoturudishia ladha za bongomuvi. 

Nimejaribu kutembelea maktaba {library} za kuuza muvi ambapo madj niliowakuta wamekiri kwamba muvi za bongomuvi zinakimbiza sokoni na haitachukua mda mrefu zitawafunika Wakorea, Wachina, Wahindi na Waturuki ambao sokoni waliongoza kwa mda wote. 

Mkojani

Chumvi Nyingi, Mkojani na Tin White ni moja kati ya wasanii walioifanya bongomuvi kufika hapo ilipo, tangu waondoke Kanumba, Mzee Majuto, Mzee Small na Sharo Milionea, akina Chumvi Nyingi wameturudishia ladha za bongomuvi. 

ALAMSIKI

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA