IHEFU SC YAHAMIA SINGIDA
Ihefu SC imehamia mkoani Singida hii ni baada ya kuuchagua uwanja wa CCM Liti kama uwanja wao wa nyumbani kwa msimu mzima.
Leo watendaji wote wa timu za ligi kuu wametumiwa taarifa rasmi ya kuwa michezo yote ya nyumbani ya Ihefu SC itachezwa CCM Liti, Singida, Taarifa ya Bodi imesema kuwa Ihefu SC itatumia uwanja wa CCM Liti Singida badala ya HIGHLAND ESTATE, Ubaruku, Mbeya.
Wakati huohuo, Singida Fountain Gate FC imeuchagua uwanja wa CCM Kirumba kama uwanja wao wa nyumbani mpaka mwishoni mwa msimu huu.