SIMBA YANUKIA ROBO FAINALI
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC usiku huu imeilazimisha Asec Mimosas sare tasa 0-0 katika uwanja wa Humphrey Felix mjini Abidjan nchini Ivory Coast na kushika nafasi ya pili nyuma ya Asec iliyofuzu robo fainali ya Ligi ya mabingwa Afrika.
Simba sasa inasubiri mchezo wake wa mwisho dhidi ya Jwaneng Galaxy utakaofanyika jijini Dar es Salaam.
MSIMAMO WA KUNDI B
1. Asec (5) — 11pts
2. Simba (5) — 6pts
3. Jwaneng (4) — 4pts
4. Wydad (4) — 3pts