VLADMIR PETROVIC KOCHA MKUU ALGERIA
Shirikisho la Soka nchini Algeria [FAF] limemteua kocha Vladmir Petrovic mwenye umri wa Miaka (60) raia wa Bosnia and Herzegovina kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya Taifa hilo akichukua nafasi ya Kocha Djamel Belmadi aliyefutwa kazi mwezi Uliopita.
Vladimir Petkovic atakuwa na kibarua cha kuisaidia timu hiyo kufuzu kwa michuano ya AFCON 2025 nchini Morocco na Kombe la Dunia la 2026 katika nchi za Mexico , Canada na Marekani, Kocha Huyo amewahi kuionoa timu ya Taifa ya Swirtzerland, na Klabu za Lazio ya Italia, Young Boys FC Sioni za Switzerland Pamoja na Bordeaux ya Ufaransa
L