KENNEDY MUSONDA: STRAIKA ANAYETUMIKA KAMA WINGA


NI mshambuliaji mwenye matumizi mazuri ya nafasi anazopata na mtekelezaji Mzuri wa majukumu anayopewa.

Mda mwingi kocha anamtumia kama winga wa kulia,Nafikiri kasi yake imemfanya Mwalimu kumtumia kwenye eneo Hilo au ule uwezo wake wa kujenga shambulizi kwa kasi kubwa au vyote kwa pamoja Mwalimu kaviona.


unapomtumia kama mshambuliaji namba mbili yaani 10 kasi yake na control yake inalazimisha sana beki kuchoka haraka mno na nihatari kwa timu pinzani akitokea Sub kwani ni ngumu sana mlinzi kumdhibiti kirahisi kwasababu yeye anaingia na kasi yake wakati mlinzi kachoka.

Anapopewa jukumu la namba 9 Musond anapenda kucheza Tisa kimvuli akizunguka eneo zima la ushambuliaji na malanyingi anaongeza nguvu kwenye viungo washambuliaji ndiyo maana ni nadra sana kumkuta kwenye mtego wa kuotea.

Kennedy Musonda
.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA