ALI KAMWE AZIMIA KWA MKAPA


WAKATI mashabiki wa Yanga wakishangilia ushindi wao baada ya kuichapa CR Belouizdad mabao 4-0 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi, hali imekuwa sio nzuri kwa ofisa habari na mawasiliano wa klabu hiyo, Ally Kamwe baada ya kuzimia.

Kamwe amekumbana na hali hiyo wakati akishangilia ushindi huo kwenye vyumba vya kubadilishia nguo akajikuta anaanguka na kupoteza fahamu.

Baada ya tukio hilo, Kamwe akachukuliwa na kutolewa nje ya uwanja kisha kuwahishwa hospitalini baada ya kupatiwa matibabu akiwa ndani ya gari la wagonjwa.

Katibu wa Madaktari wa Tiba za Wanamichezo nchini Dr Juma Sufian amethibitisha tukio hilo huku akiomba apewe muda kwani yuko kwenye harakati za kumsaidia msemaji huyo.

"Ni kweli huyu ni Kamwe amepatwa na tatizo la kupoteza fahamu, tupeni muda tumsaidie haraka ili arejee kwenye afya yake,"amesema Sufian ambaye ni daktari wa zamani wa Yanga.

Ali Kamwe

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA