PERCY TAU AWA MCHEZAJI GHALI AFRIKA



Vyanzo vikubwa vya habari Nchini Misri vimeripoti kuwa Kiungo Mshambuliaji wa Klabu ya Al Ahly,Percy Tau anatarajiwa kusaini Mkataba wa Miaka mitatu na Klabu hiyo ambapo atafanywa kuwa mchezaji anayelipwa zaidi ndani ya bara la Afrika.

Mkataba mpya wa Tau katika klabu ya Al Ahly utamfanya kutia mfukoni Mshahara wa dola milioni 5.13 katika misimu mitatu ijayo ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 13 za Kitanzania.Mshahara ya kila mwaka akiwa na Klabu hiyo ilikuwa ni dola milioni 1.2 ikiwa ni zaidi ya Shilingi Bilioni 3 kwa Mwaka na sasa itaongezeka hadi dola milioni 1.3 (zaidi ya shilingi Bilioni 3.3 za Kitanzania) katika mwaka wa kwanza, dola milioni 1.4 (zaidi ya Shilingi Bilioni 3.7) kwa mwaka wa pili na dola milioni 1.6 (zaidi ya Shilingi Bilioni 4) kwa mwaka wa tatu.

Kwenye Mkataba huo wa Tau inamaanisha Mwaka wa mwisho atakuwa anapokea Mshahara wa Shilingi Milioni 340 kwa Mwezi ambapo kwa wiki atakuwa anaramba Milioni 85,Milioni 12 kwa siku.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA