HATUTAKUWA DARAJA LA UBINGWA- MBEYA CITY
MBEYA City timu iliyopanda daraja msimu huu imetangaza vita kali na Azam FC na kudai hawatakubali kugeuzwa daraja la ubingwa kwa vinara wa ligi hiyo Azam wakati watakapokutana katika mchezo wao muhimu wa ligi kuu. Uongozi na wachezaji wa Mbeya City wamejipanga vilivyo kuhakikisha wanachukua moja ya nafasi mbili za juu ili angalau wapate kushiriki michuano ya kimataifa mwakani, lakini kama watazikosa nafasi hizo basi nguvu zao watazielekeza katika nafasi ya tatu na sivingevyo. Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mazoezi ya timu hiyo jijini Mbeya, wachezaji na viongozi hao bila kutaja majina yao wamedai wanataka kuonyesha kuwa msimu huu ni mwanzo tu ila msimu ujao mambo makubwa yanakuja kutoka kwao.