Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MOYES AAHIDI USHINDI DHIDI YA MAN CITY

David Moyes

Meneja wa Manchester United, David Moyes, amepigia klabu chake upatu kitatamba Jumanne watakapo wakaribisha majirani wao na watana shari Manchester City katika uga wao wa Old Trafford katika kivumbi cha ligi ya Premier.

Moyes alinogeshwa na ushindi wao wa 2-0 ugenini West Ham United Jumamosi na ametangaza kuwa ni ishara kuwa vijana wake wanaimarika katika wakati unaofaa.

City wanazuru Old Trafford wakiwa alama 12 mbele ya mabingwa hao waliodorora msimu huu na waliweza kuadhibu United 4-1 katika mechi ya mkondo wa kwanza katika uga wa Etihad Septemba iliyopita.

Waliendeleza harakati zao za kuridhi waasimu wao kama mabingwa pale walipocharaza Fulham 5-0 kabla ya United kujibwaga uwanjani na kuchakaza West Ham 2-0 huku kiungo Michael Carrick akicheza kama beki wa kati wa dharura kutokana na majeraha yaliokumba timu hiyo ya Moyes.


Wawili hao watakosa washambuliaji wa kutegemewa, Robin Van Persie na Sergio Aguero, wanao uguza majeraha huku United wakitazama kukosa walinda ngome muhimu, Rio Ferdinand, Johnny Evans na Chris Smalling.

“Unaweza ona kuwa tunacheza bora zaidi na imani inarejea pole pole. Tutaendelea kudhihirisha mtindo huo.
“Tulifunga matatu dhidi ya West Bromwich na Olympiakos na tumepata magoli mengine mawili hapa na wachezaji ambao hawakuonyesha uwezo wao awali katika msimu huu wanaendelea kushamiri,” Moyes alisema.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa