Ruka hadi kwenye maudhui makuu

SIMBA YAITAKA TFF IMWEKEE ULINZI TAMBWE

SIMBA SC imeliomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) liwe macho na mchezo mchafu unaotaka kufanywa na wapinzani wao katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yanga SC na Azam kwa mshambuliaji wao Mrundi, Amisi Tambwe.

Mchezo gani huo? Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Pope amesema jana kwamba magazeti yamekuwa yakiandika Yanga na Azam wanamtaka Tambwe, lakini ajabu hawajawahi kufuatwa na kiongozi yoyote wa klabu hizo.

Pope amesema kwamba kwa mujibu wa sheria za usajili, klabu yoyote inayomtaka mchezaji ambaye bado ana Mkataba na klabu yake, inatakiwa kwanza kuwasiliana na klabu yake na Tambwe amebakiza mwaka mmoja  na ushei katika Mkataba wa miaka miwili aliosaini Agosti mwaka jana.

“Ingekuwa mkataba wake umebakiza miezi sita na hajaongezewa mwingine, basi klabu nyingine zingeruhusiwa kuzungumza naye, ila huyu mchezaji atamaliza mwaka wa kwanza wa Mkataba wake Agosti mwaka huu.


Kwa hivyo unaweza kuona ni kosa kwa kiongozi wa klabu yeyote kujaribu kufanya naye mazungumzo ya kumshawishi na kanuni za adhabu zipo, sasa sisi tunaiomba TFF iwe makini na mchezo wowote mchafu unaotaka kufanywa na wapinzani wetu,”alisema Poppe akiwa safarini kuelekea Japan jana kwa shughuli zake za kibiashara.

Alipoulizwa kama iwapo watapelekewa ofa na moja ya wapinzani wao hao katika Ligi Kuu, Poppe alisema watakuwa tayari kuwasikiliza, ila akawaambia kabisa dau la kuanzia la mauzo ya mchezaji huyo ni dola za Kimarekani 350,000.

“Ndiyo, sisi hatushuki chini, Okwi (Emmanuel) tulimuuza dola 300,000 Etoile du Sahel (ya Tunisia), hivyo na Tambwe hatuwezi kumuuza chini ya bei hiyo, atakayefika bei tutampa huyo mchezaji, sisi tutaleta mkali mwingine,”alisema Pope.

Tahadhari; Hans Poppe amezionya Yanga na Azam zisithubutu kuzungumza na Tambwe, wakifanya hivyo watakuwa wamevunja sheria za usajili na ameiomba TFF iwe macho dhidi ya mchezo mchafu.

Hadi sasa, Tambwe amekwishaichezea Simba SC mechi 23 katika mashindano yote na kuifungia mabao 19, kati ya hayo 17 amefunga katika Ligi Kuu na kumfanya aongoze kwenye mbio za ufungaji bora kwa mabao manne zaidi dhidi ya Kipre Tchetche wa Azam anayemfuatia.

Okwi aliuzwa Tunisia, lakini hadi sasa Simba SC haijalipwa fedha zake na Etoile, wakati mchezaji huyo alivurugana na klabu hiyo akidai alikuwa halipwi mishahara, hivyo kufungua kesi Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

FIFA ilimruhusu kujiunga na timu nyingine wakati kesi yake ikiendelea naye akaenda SC Villa ya kwao,Uganda kabla ya Desemba mwaka jana kutua Yanga SC anakoendelea na kazi hivi sasa.

Wakati Simba SC inadai fedha zake Etoile, klabu hiyo ya Tunisia nayo imefungua kesi mpya FIFA, safari hii ikitaka kulipwa fidia ya Euro Milioni 1.5 sawa na Sh. Bilioni 3.1 za Tanzania.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa