HATUTAKUWA DARAJA LA UBINGWA- MBEYA CITY
MBEYA City timu iliyopanda daraja msimu huu imetangaza vita kali na Azam FC na kudai hawatakubali kugeuzwa daraja la ubingwa kwa vinara wa ligi hiyo Azam wakati watakapokutana katika mchezo wao muhimu wa ligi kuu.
Uongozi na wachezaji wa Mbeya City wamejipanga vilivyo kuhakikisha wanachukua moja ya nafasi mbili za juu ili angalau wapate kushiriki michuano ya kimataifa mwakani, lakini kama watazikosa nafasi hizo basi nguvu zao watazielekeza katika nafasi ya tatu na sivingevyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mazoezi ya timu hiyo jijini Mbeya, wachezaji na viongozi hao bila kutaja majina yao wamedai wanataka kuonyesha kuwa msimu huu ni mwanzo tu ila msimu ujao mambo makubwa yanakuja kutoka kwao.
Wamedai Azam haitatoka na pointi tatu katika uwanja wa Sokoine isipokuwa watafungwa ama sare,tutacheza mchezo wetu wa kujituma mwanzo mwisho ili tuweze kuwadhibiti Azam ambao wanataka kutugeuza daraja laola kupatia ubingwa wa bara.
Mchezo huo kati ya Azam na Mbeya City unatajwa kutoa picha ya ubingwa kwa Azam ambayo inaongoza kwa pointi 50 huku Yanga ikifuatia kwa karibu ikiwa na pointi 46 na Mbeya City yenyewe ina pointi 42, nini kitatokea katika mpambano wao, tusubiri kisha tuone