LOGARUSIC MGUU NDANI MGUU NJE SIMBA
Wakati kikosi cha Simba kikiendelea kupata matokeo yasiyoridhisha katika mechi za Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara inayoendelea, Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic, amesema yuko njia panda kutokana na kutojua hatma yake ndani ya klabu hiyo.
Mcroatia huyo aliyejiunga na Simba Desemba mwaka jana baada ya kuitumikia Gor Mahia ya Kenya, anamaliza mkataba wake wa awali wa miezi sita Mei 31, mwaka huu.
Awali Kamati ya Utendaji ya Simba ilitaka kumuongeza mkataba kocha huyo lakini baadaye ikaamua kusitisha kufuatia muda wao wa kukaa madarakani kubakia mchache.
Hata hivyo, chanzo chetu ndani ya Simba kimeeleza kwamba wamesitisha rasmi mchakato wa kumpa Loga mkataba mpya na kwamba zoezi hilo litafanywa na uongozi mpya kama utaona anastahili.
"Unajua kumpa mkataba mpya halafu uongozi mpya usiporidhishwa naye ni kuibebesha klabu mzigo wa kumlipa kwa kuvunja mkataba naye, hivyo Mei siyo mbali, ukiingia madarakani utaamua," kilieleza.
Akizungumza mtandao huu, Logarusic, alisema kutojua hatma yake ndani ya Simba ni jambo linalomtesa na kufafanua kuwa anashindwa kufanya baadhi ya maamuzi na maandalizi ya timu mojawapo ikiwa ni kuanza kwa mchakato wa usajili wa wachezaji kwa ajili ya msimu ujao.
"Siwezi kuzungumzia mipango mingine kwa sababu sijui hatma yangu, nitakuwapo au sitakuwapo," alisema kwa kifupi kocha huyo.
Katibu Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga, akizungumzia suala la mkataba wa Loga, alisema kwamba bado uongozi wa klabu hiyo unaomaliza muda wake Mei 4, mwaka huu haujafikia maamuzi ya mwisho yanayohusiana na mkataba wa kocha huyo.