OBAMA AICHIMBA MKWARA URUSI
Rais wa Marekani Barrack Obama,
ameonya Urussi kusitisha mpango wake wa kutaka kutwaa eneo la Crimea
nchini Ukraine lasivyo iwekewe vikwazo.
Bwana Yatsenyuk amesema taifa lake sasa ni sehemu ya mataifa ya Magharibi na kamwe haliwezi kurudi nyuma.
Mabalozi katika Umoja wa Mataifa, wanasema Mataifa ya Magharibi yanaandaa azimio la pamoja, katika baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo litakariri uhuru wa taifa la Ukraine na pia kuangazia kuhusu kura ya maoni kuhusu itakayofanyika siku ya Jumapili, ikiwa eneo hilo la Crimea litajitenga na kuwa sehemu ya Urussi.
Hata hivyo inatarajiwa kuwa Utawala wa Moscow utatumia kura yake ya turufu katika baraza hilo la Umoja wa Mataifa kupinga azimio hilo.