LOGA AITABIRIA UBINGWA YANGA.

Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic ‘Loga’ amesema tiketi ya timu yake kufuzu kucheza michuano ya kimataifa ipo mikononi mwa Azam FC, Yanga na Mbeya City.

Awali, Loga ambaye alijiunga na kikosi cha Wekundu hao wa Msimbazi Desemba mwaka jana, aliweka wazi kwamba kikosi chake hakina nafasi ya kutwaa ubingwa msimu huu.

Kwa sasa Simba inakamata nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 36, baada ya kucheza mechi 21, kati ya hizo kushinda tisa, kutoka sare tisa na kupigwa mara tatu,  kama Simba watashinda mechi zake zote tano itafikisha pointi 51.

Azam FC inakamata uongozi wa ligi hiyo ikiwa na pointi 40 wakiwa na mechi nne mkono, Mbeya City ni ya pili ikiwa na pointi 39 na Yanga ni ya tatu ikiwa na pointi 38.

Hata hivyo, Yanga inapewa nafasi zaidi ya kunyakua taji hilo kutoka kutokana na kusaliwa na michezo mitano  mkononi.


Loga alisema: “Sina uhakika kama tutashiriki mashindano ya kimataifa au la kwa sababu tulifanya makosa makubwa kupoteza mechi mbili.

“Ok, tuna uwezo wa kushinda mechi zote zilizosalia, lakini hiyo pekee haiwezi kutupa nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa isipokuwa pale tu wenzetu walioko juu yetu watakapovurunda,” alisema Loga

Aliongeza: “Tutakachofanya sisi ni kupambana hadi mwisho baada ya hapo  tutajua nafasi yetu,” alisema Loga ambaye anasemekana ataikacha Simba mwisho wa msimu wakati mkataba wake wa miezi sita utakapofikia ukingoni.

Katika hatua nyingine, Loga alisema ataendelea kusimamia misingi ya taaluma yake licha ya kwamba anafahamu wapo wasiofurahishwa.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA