MWAKA WA TAABU KWA WAINGEREZA, SPURS YABUTULIWA NYUMBANI 3-1

KLABU ya Tottenham Hotspur imeanza vibaya hatua ya 16 Bora ya Europa League baada ya usiku wa jana kuchapwa mabao 3-1 nyumbani Uwanja wa White Hart Lane, London na Benfica ya Ureno.

Ni pigo lingine kwa Waingereza wa England baada ya Manchester City na Arsenal kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, Spurs wanachungulia mlango wa kutokea kwenye michuano hiyo ya Ulaya.

Spurs sasa inatakiwa kufanya maajabu ambayo yamewashinda City na Arsenal kwenda kushinda ugenini mabao 3-0 ili kusonga mbele.

Mabao ya Wareno yalifungwa na Rodrigo dakika ya 30, Luisao dakika ya 58 na 84 wote pasi za Ruben Amorim, wakati bao la Spurs lilifungwa na Eriksen dakika ya 64.


Katika mechi nyingine jana, Valencia iliifunga 3 – 0 Ludogorets, Napoli ilifungwa 1-0 nyumbani na Porto, Basel ililazimishwa sare ya bila kufungana na Salzburg nyumbani, Anzhi ilifungwa 1-0 nyumbani na AZ, Viktoria Plzen imefungwa 4-1 nyumbani na Olympique Lyon, Fiorentina imetoka sare ya 1 – 1 na Juventus na Real Betis imeilaza 2-0 Sevilla

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA