KANYE WEST AHUKUMIWA KIFUNGO CHA NJE
Mwanamuziki wa muziki wa kufoka
au Rap nchini Marekani Kanye West, hajakana wala kukubali mashitaka ya
kumshambulia mpiga picha katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Los
Angeles.
Mpiga picha Paparazzi ,Daniel Ramos, alimtuhumu muimbaji huyo kwa kumpiga makonde na kumpokonya kamera yake.
Muimbaji huyo mwenye umri wa miaka 36 anasisitiza kuwa hana hatia.
"nilikuwa nafanya kazi yangu wakati West aliponishambulia, '' alisema mpiga picha huyo, '' ikiwa ni mimi ningekuwa nimemfanyia kitendo hicho ningekuwa kizimbani.''
Ramos pia alidai kuwa alihofia kulipiza kisasi baada ya matamshi ya muimbaji huyo kupitia kwenye televisheini.
West alikamatwa mwaka 2008 kufuatia vurumai lengine na mpiga picha katika uwanja huohuo wa ndege.
Kesi hiyo, ilitupiliwa mbali na mahakama baada ya West kuwalipia vifaa vilivyoharibika na pia kupata ushauri nasaha kuhusu namna ya kudhibiti hasira zake.