MOTO WAITEKETEZA BAA YA HIGHLAND TABATA BARACUDA

MOTO mkubwa uliotokea asubuhi ya leo umeweza kuiteketeza kabisa bar maarufu ya Highland Night Park iliyopo Tabata Baracuda iliyo pembezoni mwa barabara iendayo Vingunguti na kusababbisha uahiribu mkubwa wa mali.

Mwandishi wetu alikuwepo kwenye tukio ambapo inasemekana chanzo cha kutokea moto huo ni shoti ya umeme, jitihada za majirani zilishindakana kuokoa mali zilizokuwemo ndani ya bar hiyo licha ya kufanikiwa kuwaokoa watu na hakuna majeruhi hata mmoja.


Moto huo uliopamba asubuhi na mapema uliweza kuangamiza maeneo ya paa na kusababisha vitu vingine kuungua moto hivyo kuweza kuipoteza kabisa bar hiyo ambayo imekuwa ikitumiwa na watu mbalimbali jijini kama sehemu ya kupumzikia siku za wikiendi

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA