KOCHA WA GHANA ATUA LIVERPOOL
Appiah pamoja na kocha wa golkipa Nassam Yakubu, watajionea Liverpool inavyofanya maandalizi kabla ya michuano yoyote.
Zaidi ya hayo kocha huyo wa Black stars, atakutana na maafisa wa shirikisho la mameneja katika uwanja wa St. George, kituo cha mazoezi ya timu ya taifa ya soka ya England.
Ziara hii inalenga kusaidia maandalizi ya timu ya taifa ya Ghana kabla ya kushiriki michuano ya kombe la dunia.
Ujumbe huo unajumuisha naibu wa Appiah, Maxwell Konadu, Yakubu, daktari wa kikosi hicho, Adam Baba na mdadisi Michael Okyere.
Wanatarajiwa kuondoka Accra hii leo kwa ziara hiyo itakayodumu siku kumi.
"hii ni fursa nzuri sana kwetu kuweza kutembelea Liverpool,moja ya vilabu mahiri vya soka duniani kujionea wanavyojiandaa kabla ya michuano,'' alisema Rais wa shirikisho la soka nchini Ghana Kwesi Nyantakyi.
"bila shaka fursa hii itakua muhimu sana kwa kikosi cha Black Stars na itawasaidia kuleta nyumbani ushindi.''
Sio mara ya kwanza kwa Appiah kuzuru England ili kuboresha uzoefu wake na wa wachezaji, amewahi kutembelea Manchester zaidi ya mara moja.
Ghana iko katika kundi G katika michuano ya kombe la dunia pamoja na Brazil na Ujeumani , Ureno na Marekani.