MATOLA AWALILIA OKWI, YONDANI, KASEJA SIMBA, ADAI PENGO LAO BADO LINAWATESA
Kocha msaidizi wa timu ya Simba, Selemani Matola, amesema kuwa mabadiliko yaliyofanywa katika benchi la ufundi la timu hiyo ndiyo yalisababisha kikosi hicho kupotea kwenye mbio za kusaka ubingwa wa msimu huu wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara ambayo inatarajiwa kumalizika Aprili 19 mwaka huu.
Msimu uliopita Simba ilimaliza ligi ikiwa na Mfaransa Patrick Liewig, ambaye alitimuliwa na nafasi yake kuchukuliwa na mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Abdallah Kibaden 'King' ambaye naye aliondolewa na mikoba yake ikarithiwa na Mcroatia Zdravko Logarusic.
Akizungumza jana, Matola, alisema kuwa mabadiliko hayo yaliifanya timu ianze mchakato wa kusaka kikosi cha kwanza wakati ligi ikiwa tayari imeanza.
Matola alisema kuwa kila mwalimu huwa na sera zake na vile vile kuondoka kwa nyota wakongwe (Juma Kaseja, Juma Nyoso, Haruna Moshi 'Boban', Kelvin Yondani na Emmanuel Okwi) kuliwafanya wachezaji waliobakia "kutojiamini" kuitumikia klabu hiyo hadi pale walipoona mashabiki na viongozi wameanza kuridhishwa na viwango vyao.
"Ila bado tunatakiwa kuheshimu na kuthamini vipaji vyetu, kama ile timu yangu iliyochukua ubingwa kwa BancABC ingeendelea kutunzwa, sasa hivi tungekuwa tunazungumzia mambo mengine," alisema nahodha huyo wa zamani wa Simba.
Aliongeza kuwa kila mchezaji sasa anapaswa kujituma na kuhakikisha Simba inalinda heshima kwa kupata matokeo mazuri kwenye mechi zilizobaki.
"Ligi ni ngumu na inakuwa ngumu zaidi pale tunapocheza dhidi ya timu ndogo, enzi zetu haikuwa hivi, sasa hivi timu ndogo zimezidi kukaba na kuonyesha uwezo wao dhidi ya timu za Dar es Salaam," Matola aliongeza.
Aliwataka wanachama na mashabiki wa Simba kuwa pamoja na kuanza kujenga kikosi cha msimu ujao.
Alieleza pia haoni sababu ya kusajili wachezaji wa kigeni wakati rasilimali kutoka katika timu ya vijana ipo na inachotakiwa kufanya na kuwapa maandalizi sahihi na kuacha kuandaa timu pale inapokaribia mashindano.
Msimu uliopita Simba ilimaliza ikiwa ya tatu katika msimamo wa ligi nyuma ya mabingwa Yanga na Azam na hivyo ilikosa nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa mwaka huu.
Hali hiyo huenda pia ikajirudia mwakani ingawa lolote linaweza kutokea katika soka