OBAMA KUKUTANA NA PAPA FRANCIS
Rais Barrack Obama wa Marekani
anatarajiwa kukutana na kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa
Francis, katika makao yake makuu huko Vatican.
Wawili hao wanatarajiwa kujadili namna ya kupunguza tofauti iliyopo kati yao katika maswala mengi mbali na kujaribu kuinua maisha ya watu maskini duniani baada ya takwimu kuonyesha kuwa tofauti ya mapato kati ya matajiri na Masiki inaendelea kupanuka .
Aidha viongozi hao wawili wanatazamiwa kujadili hali ilivyo Nchini Ukraine, na swala la upatikanaji wa amani mashariki ya kati.
Mwafaka baina ya mitazamo tata kuhusiana na maswala ya uavyaji mimba, matumizi ya dawa za kupanga uzazi na ndoa ya jinsia moja pia inatarajiwa kuwa kati ya mada itakayojadiliwa .