ROONEY ADAI JINAMIZI LAZIDI KUWAANDAMA
Mshambulizi wa Manchester United
Wayne Rooney amesema kuwa kipigo cha mabao 3-0 walichokipata kutoka kwa
Liverpool ni kama janga kwake na hiki ndio kipindi kigumu kwake kuwahi
kukishuhudia tangu kuanza kucheza soka ya kulipwa.
Rooney mzaliwa wa Liverpool mwenye umri wa miaka 28, amesema kuwa hiki ni kipindi kigumu sana kwake na wembe ambao hautoshi hata kumezwa.
"hili ni jinamizi . Ni siku mbaya sana kwangu , sijawahi kuhisi vibaya hivi maishani mwangu nikicheza soka.
''Yaani hata ni vigumu kutafakari. Liverpool ilicheza vyema sana , lakini hii ni hali ngumu kwangu, '' alisema Rooney
''Hakuna anayetaka kushindwa hapa hasa katika uwanja wa nyumbani, sio vizuri.''
Rooney,aliyesaini mkataba mpya na klabu hiyo, mwezi jana , alipata tu fursa moja ya kujaribu kuingiza bao katika mechi hiyo ambayo Liverpool ilidhibiti tangu mwanzoni ingawa hakufanikiwa
Man U wanashikilia nafasi ya saba katika jedwali la pointi , ingawa Rooney anayepokea mshahara wa pauni laki tatu kwa wiki amesema kuwa hajafa moyo sana kutokana na matokeo mabaya ya Manchester United.
Kocha wa klabu hiyo David Moyes amesema kuwa aliachwa kinywa wazi asijue la kusema.