SIMBA KUTIBUA NDOTO ZA AZAM KUTWAA UBINGWA WA BARA JUMAMOSI
Majaliwa ya Yanga na Azam FC kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara yapo mikononi mwa Simba ambayo imebakiza mechi na vigogo hivyo vinavyofukuzana kwa karibu katika msimamo wa ligi hiyo inayotarajiwa kumalizika Aprili 19, mwaka huu.
Azam ambayo ipo kileleni ikiwa na pointi 47, nne zaidi ya Yanga inayoshika nafasi ya pili, imebakiza mechi nne huku wapinzani wao wakibakiza tano, lakini zote zitalazimika kukutana na Simba, hivyo kupoteza dhidi ya Kikosi hicho cha Zdravko Logarusic kwa timu hizo kunaweza kupeperusha ndoto za kutwaa ubingwa.
Hata hivyo, Azam italazimika kuanza kushinda Jumamosi dhidi ya Simba kabla ya kujipanga kuibuka na ushindi itakapokutana na Ruvu Shooting ugenini na baadaye kuikabili Mbeya City kabla ya kumaliza na JKT Ruvu.
Wakati Yanga yenyewe itakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Tanzania Prisons kesho Taifa na Jumamosi kuifuata Mgambo JKT Uwanja wa Mkwakwani na baadaye kurudi Taifa kuialika JKT Ruvu.
Baada ya mechi hiyo, itasafiri kuifuata Oljoro JKT katika Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid na kisha kumaliza na Simba Taifa.
Hata hivyo, kikwazo kingine cha Azam kinaweza kuwa Mbeya City ambayo ina kumbukumbu ya kupoteza mechi moja tu katika Uwanja wao wa Sokoine.
Tayari mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, Yanga, jana jioni waliingia kambini katika jengo la makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo mtaa wa Jangwani na Mafia kwa ajili ya kujiandaa na mechi yao ya kesho dhidi ya Prisons kutoka jijini Mbeya.
Yanga imeamua kurejea kwenye makao makuu badala ya Bagamoyo kama ilivyotangaza kuwa ndiyo kambi yao ya kudumu msimu huu.
Kocha Msaidizi wa Yanga, Boniface Mkwasa, alisema kikosi hicho sasa hakitakuwa na mapumziko kwa sababu mechi zote zilizobakia ni ngumu na wao wanahitaji ushindi.Mkwasa alisema katika mbio za ubingwa hawapo peke yao, hivyo hawatakiwi 'kushangaa'.
"Hakuna kulala, tunajua kwamba sio peke yetu tunaotaka kikombe cha ubingwa, tunaendelea na mazoezi hakuna kupumzika," alisema kocha huyo wa zamani wa Ruvu Shooting.
Alisema kwamba Yanga imejiandaa kukutana na changamoto mbalimbali na ushindani kutoka kwa timu pinzani.
Aliongeza kuwa ligi ni ngumu na kila mchezaji anapaswa kujituma ili waweze kufikia malengo.