TAMBWE AAHIDI KUFIKISHA MAGOLI 22 LEO

MSHAMBULIAJI wa kutegemewa wa klabu ya Simba Amissi Tambwe leo ameahidi kufikisha magoli 22 wakati klabu yake ya Simba itakapomenyana na Coastal Union ya Tanga katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kauli hiyo ameitoa mapema leo wakati wa maandalizi ya mchezo huo ambapo amedai anataka kutoka na magoli matatu mguuni kwake ili afikishe magtoli 22, lakini endapo itashindikana anataka kufunga goli moja, aidha amesisitiza ndoto yake msimu huu ni kufikisha magoli 25.

Akizungumza kwa upole zaidi Tambwe amedai kiola mechi kwake ni fainali na anataka kufunga, Simba iliyo katika nafasi ya nne ikipigania nafasi ya pili au ubingwa inakabiliana vikali na Coastal Union ya Tanga ambayo hivi karibuni ilipokea kipigo cha mabao 4-0 toka kwa Azam FC.

Mchezo wa leo hautakuwa rahisi kwa Simjba kuchomoza na ushindi kwani vijana wa Coastal wanaonekana kuupania mchezo wa leo ili watoke na pointi tatu muhimu, beki wa kutumainiwa aliyemo kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars Abdi Banda amesema anataka kuwaonyesha Watanzania kuwa hawakukosea kumwita Stars.


Banda mtoto wa beki wa zamani wa Simba Hassan Banda amesema kuwa atamkaba vilivyo Tambwe na kamwe hatofurukuta katika mchezo huo, naye kocha msaidizi wa Simba Seleman Matola ametamba kuibuka na ushindi katika mchezo huo, Matola amedai kuwa kikosi chake kimeimarika zaidi 

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA