Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MAN UNITED YAZIDI KUMUUMIZA KICHWA MOYES, YAPIGWA 3-0 NA VIJOGOO

KLABU ya Manchester United imeizawadia ushindi wa kwanza Liverpool Uwanja wa Old Trafford baada ya miaka mitano, kufuatia kuchapwa mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.

Kiungo Steven Gerrard amefunga mabao mawili kwa penalti dakika za 34 na 46 wakati Luis Suarez amefunga bao lake la 25 msimu huu dakika ya 84 kukamilisha ushindi mnono wa 3-0.Gerrard alifunga penalti ya kwanza baada ya beki wa United, Rafael kuunawa mpira kwenye eneo la hatari na Nahodha huyo wa Wekundu wa Anfield akafunga tena kwa tuta lingine kufuatia Phil Jones kumchezea rafu Joe Allen kipindi cha pili.

Nahodha huyo wa England angeweza kuifungia Liverpool hat-trick ya kwanza Old Trafford tangu mwaka 1936 kama mkwaju wake wa tatu wa penalti usingegonga mwamba baada ya Nemanja Vidic kumchezea rafu Daniel Sturridge.


Vidic alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa rafu hiyo - hiyo ikiwa mara ya nne anatolewa kwenye mechi dhidi ya Liverpool, ingawa marudio ya picha za Televisheni yalimuonyesha Sturridge akijirusha ili kupata penalti.

Matokeo hayo yanaifanya Liverpool itimize pointi 62 baada ya mechi 29 na kupanda nafasi ya pili, ikiishusha Manchester City yenye pointi 60 za mechi 27 katika nafasi ya nne na Arsenal yenye pointi 62 za mechi 29 sasa ni ya tatu, Chelsea ikiendelea kuongoza kwa pointi zake 66 za mechi 30.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa