Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MESSI NOOMA APIGA HAT TRICK BARCA IKIUA 7-0 LA LIGA

MSHAMBULIAJI Lionel Messi amefunga mabao matatu katika ushindi wa 7-0 wa Barcelona dhidi ya Osasuna Uwanja wa Camp Nou kwenye mchezo wa La Liga jana.

Messi sasa anaweka rekodi nyingine kwa hat-trick hiyo, akiwa mfungaji bora wa kihistoria Barcelona kwenye mashindano yote, baada ya kufikisha mabao 371 akimpiku Paulino Alcantara.

Messi pia sasa amebakiza bao moja kumfikia gwiji wa zamani wa Real Madrid, Hugo Sanchez kwa ufungaji bora kwenye historia ya La Liga. Anaweza kumpiku Sanchez wiki ijayo katika dhidi ya mahasimu, Real Madrid Uwanja wa Santiago Bernabeu.

Muargentina huyo alifungua biashara leo dakika ya 18 akimalizia pasi ya Alexis Sanchez ambaye alifunga la pili dakika ya 22 kwa pasi ya Jordi Alba kabla ya Andres Iniesta kufunga la tatu dakika ya 34 kwa pasi ya Sergio Busquets.


Kipindi cha pili, Messi tena alifungua biashara dakika ya 63 kwa pasi ya Iniesta aliyetoa pia na pasi ya bao la tano lililofungwa na Tello dakika ya 78.

Messi akaurudisha mpira nyavuni tena dakika ya 88 kukamilisha hat trick yake kwa pasi ya Dani Alves kabla ya kutoa pasi ya bao la saba kwa Pedro dakika ya 90.

Barcleona sasa inabaki inazidiwa pointi nne Real Madrid katika mbio za ubingwa La Liga.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa