MABEKI WANANIKAMIA SANA- OKWI
Ukame wa kucheka na nyavu unamtesa mshambuliaji wa Kimataifa wa Yanga kutoka Uganda, Emmanuel Okwi, lakini amejitetea kuwa bado kiwango chake cha kucheza soka kiko juu licha ya kutofunga mabao kwenye mechi za Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara inayoendelea.
Yanga ilimsajili Okwi kwa gharama ya zaidi ya milioni 100 akitokea SC Villa ya Uganda ambayo ilipewa kibali cha kumtumia kufuatia kutofautiana na klabu yale ya Etoile Sportive du Sahel ya Tunisia.
Okwi alifunga bao moja wakati mabingwa hao watetezi wakipata ushindi wa 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting na akafunga tena kwa penalti walipokuwa Alexandria wakirudiana na Al Ahly kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika mapema mwezi huu.
Akizungumza Okwi, alisema kuwa anapokuwa uwanjani kila mchezaji wa timu pinzani anajipanga kumzuia yeye ili asiweze kuutawala mchezo.
Okwi ambaye pia ni mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) alisema licha ya kutofunga, mchango wake kwenye timu unaonekana na anafurahia kuona Yanga bado ina uwezo wa kutetea ubingwa msimu huu.
Alisema ligi ni ngumu lakini anaamini wachezaji wa Yanga watapambana kuhakikisha wanamaliza msimu kwa kupata kikombe hicho cha ubingwa wa Bara.
"Ligi ni ngumu na ina ushindani, hakuna mechi rahisi kwa sababu kila timu inajiandaa kusaka ushindi," alisema mchezaji huyo.
Mganda huyo Jumamosi alitoa pasi iliyozaa bao la tatu lililofungwa na Hussein Javu katika ushindi wa 3-o walioupata Yanga kwenye Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mkoani Tabora dhidi ya Rhino Rangers.
Baada ya kurejea kutoka mkoani Tabora juzi usiku, Yanga iliingia kambini jana jioni katika makao makuu ya Klabu yao yaliyopo mtaa wa Twiga Jangwani kujiandaa na mechi ya kesho dhidi ya Prisons kutoka ya Mbeya.
Okwi atakumbukwa na mashabiki wa Simba kutokana na kuifungia timu hiyo na kuonyesha kiwango cha juu wakati ilipoibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Yanga.