RAMADHANI SINGANO KUADHIBIWA NA SIMBA

SIMBA SC imesema haitamuacha hivi hivi kiungo wake mshambuliaji, Ramadhani Yahya Singano ‘Messi’ anayedaiwa kuvunja kioo cha mlango wa chumba cha kubadilishia nguo cha timu yake jana, ikiahidi kumchukulia hatua za kinidhamu.

Mchezaji huyo anayeishi Keko Machungwa, Dar es Salaam anadaiwa kuvunja kioo hicho Uwanja wa Taifa, Jijini hapa baada ya mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union ya Tanga, timu yake ikifungwa 1-0.

“Viongozi walikutana jana, walilijadili hilo suala, kwa sasa siwezi kusema lolote, ila ni wazi lazima Messi atachukuliwa hatua, hataachwa hivi hivi,”alisema Ofisa Habari wa klabu hiyo, Asha Muhaji leo alipozungumza.

 
Pamoja na ushahidi uliotolewa na wafanyakazi wa Uwanja wa Taifa kwa askari Polisi kwamba, Messi ndiye aliyevunja kioo, hicho lakini wachezaji wenzake na viongozi wa Simba SC walimtetea.

Polisi jana walishindwa kuchukua hatua yoyote kuhofia kusababisha vurugu na mchezaji huyo aliondoka uwanjani hapo kuelekea kwenye basi la timu yake akisindikizwa na baunsa.

Tukio hilo limechukuliwa kama hasira za kipigo cha bao 1-0 nyumbani mbele ya Coastal Union katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI