MAN CITY HAISHIKIKI ENGLAND
MANCHESTER City imerudi kwa hasira katika Ligi Kuu ya England ikitoka kutolewa Ligi ya Mabingwa Ulaya- baada ya jana jioni kuifumua mabao 5-0 Fulham katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Etihad mjini Manchester.
Mwanasoka Bora wa Afrika, Yaya Toure jana amepiga hat trick yake ya kwanza, mabao mawili akifunga kwa penalti dakika ya 26 na 54 na lingine dakika ya 65 akimalizia pasi ya Samir Nasri.
Mabao mengine ya Man City yamefungwa na Fernandinho dakika ya 84, akimalizia pasi ya Milner na Demichelis dakika ya 88. Ushindi huo, unaifanya City ifikishe pointi 63 baada ya kucheza mechi 28 na kupanda nafasi ya tatu mbele ya Arsenal yenye pointi 62 za mechi 30.
Chelsea inaongoza Ligi Kuu England kwa pointi zake 69 za mechi 31, ikifuatiwa na Liverpool yenye pointi 65 baada ya mechi 30, wakati Arsenal yenye pointi 62 ni ya nne.