MTIBWA SUGAR WAAPA KUITIBULIA YANGA YA MISRI

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

WAKATA miwa wa Mtibwa Sugar wenye maskani yao Tuliani Manungu wilayani Mvomelo mkoani Morogoro ambao kesho Jumamosi wataikaribisha Yanga ya 'Misri' katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wameapa kuitibulia rekodi timu hiyo kwa kuifunga.

Akizungumza na Mambo Uwanjani, msemaji wa timu hiyo Tobias Kifaru amesema kuwa kikosi chake kina rekodi nzuri ya kuifunga Yanga hivyo kesho kitalinda heshima yake, ameongeza kuwa Yanga hii ya sasa yenye uwezo wa kushinda magoli 7-0 na kuivimbia timu kubwa na mabingwa wa Afrika Al Ahly ya Misri lakini jeuri yao imekwisha.

Kifaru analingia ushindi wa mabao 3-0 ilioupata mwaka juzi katika mzunguko wa kwanza, naye kocha wa Mtibwa Sugar Meck Mexime ametamba kuibuka na ushindi katika mchezo huo, 'Yanga ni timu ya kawaida kama nyingine hivyo sioni sababu ya kuiogopa' alisema Mexime.


Yanga inashuka dimbani kesho kuikabili Mtibwa Sugar ambayo inafanya vibaya katika ligi kuu ya Vodacom mzunguko wa pili,hadi sasa Yanga inakamata nafasi ya tatu ikiwa na pointi 38 lakini ndio timu yenye iliyosaliwa na mechi nyingi zaidi msimu huu

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA