MO FARAH ATETEA MAAMUZI YAKE
Mwanariadha wa Uingereza,
mzaliwa wa Somalia Mo Farah, amekariri kuwa alifanya uamuzi bora
kushiriki katika mashindano kadhaa ya barabarani kabla ya kushiriki
katika mbio za London Marathon mwezi ujao.
Farah atakuwa miongoni mwa wanariadha watakaoshiriki katika mbio za kilomita ishirini na moja mjini New York Jumapili hii.Mwanariadha mashuhuri wa Ethiopa, Haile Gebrselassie alikuwa amesema ni mapema sana kwa Farah mwenye umri wa miaka 30 kushiriki katika mbio hizo za marathon, na badala yake kutoa ushauri kwake kuipa mashindano ya uwanjani nafasi ya kwanza.