MAAJABU: MAN UNITED YATINGA ROBO FAINALI ULAYA

MAAJABU yamewezekana. Manchester United imekuwa timu ya pili ya England kutinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ikiungana na Chelsea baada ya Arsenal na Manchester City kutolewa.

Hiyo inafuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Olympiacos ya Ugiriki jana usiku Uwanja wa Old Trafford, ambao unawafanya wasonge mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2, baada ya awali kufungwa 2-0 ugenini.

Van Persie alifunga bao la kwanza kwa penalti, baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu katika eneo la hatari, wakati la pili alifunga akiunganisha krosi ya Wayne Rooney na la tatu kwa mpira wa adhabu.

Man United na Dortmund, sasa zimeungana na Real Madrid, Bayern Munich, Barcelona, Atletico Madrid, Chelsea na PSG katika hatua hiyo, ambayo droo yake itapangwa baadaye mwezi ujao.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA