ANDRE MARRINER ALIKOSEA KUTOA KADI NYEKUNDU: FA


Wachezaji wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain na Kieran Gibbs wameondolewa adhabu ya kadi nyekundu baada ya Gibbs kuondolewa uwanjani kimakosa wakati wa mchuano wa siku ya Jumamosi ambapo Arsenal ilishindwa vibaya na Chelsea kwa kipigo cha magoli 6-0 uwanjani Stamford Bridge.

Jopo la chama cha soka England, FA, limesema kuwa refa Andre Marriner alikosea kwa kumtimua uwanjani Kieran Gibbs na kwamba tukio la Oxlade-Chamberlain kuunawa mpira katika eneo la hatari haikustahili kadi nyekundu.


Sasa wachezaji hao hawatahudumia marufuku ya mechi kutokana na tukio hilo.
Maafisa wa usimamizi wa mechi walisema kuwa refa huyo mwenye umri wa miaka 43, ambaye tayari ameomba msamaha kwa kukanganya majina ya wachezaji, anapaswa kupewa fursa nyingine kurekebisha makosa yake badala ya kunyimwa kibarua mwishoni mwa juma hili.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA