Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2014

ETO'O KUENDELEA KUTESA CHELSEA

Picha
Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho, ametangaza kuna uwezekano nyota wa Cameroon, Samuel Eto’o, atasalia katika klabu hicho msimu ujao licha ya habari anakusudia kurejea Uhispania kandarasi yake itakapoisha Juni. Mourinho anakusudia kumhifadhi mshambulizi huyo wa zamani wa Mallorca na Barcelona, 32, lakini anasema uamuzi wa mwisho uko mikononi mwa klabu ama Eto’o musimu utakapo karibia kuyoyoma. Eto’o ameibuka mshambuliaji kigezo wa timu hiyo huku Fernando Torres akiendelea kuuguza jeraha la goti huku kampeni ikizidi kuchacha moto.

EMMANUEL OKWI ANUKIA MSIMBAZI

Picha
MGANDA Emmenuel Okwi aliyesajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili na nusu kukipiga Yanga kabla na shirikisho la kandanda nchini TFF kuingilia kati kuhoji usajili wake kama una baraka zozote kutoka Fifa, Imebainika kuwa mchezaji huyo atarejeshwa katika klabu yake ya zamani ya Simba endapo klabu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia itashiondwa kuilipa Simba SC pesa zake dolaza Kimarekani 300,000. Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari ambaye ni rafiki wa karibu na mjumbe mmoja wa kamati ya sheria, hadhi za wachezaji wa TFF amedai kuwa barua iliyoandikwa na TFF kwenda Fifa ilikuwa na nmaaguizo mawili tu.

UNYAMA MTUPU: KIJANA AUAWA MCHANA KWEUPEE, AHUSISHWA NA 'UASI' TABATA.

Picha
Na Salum Fikiri Jr HALI imeanza kuwa mbaya hasa jijini Dar es Salaam na vitongoji vyake, wananchi wenye hasira kali waishio Tabata Mtambani wamempiga mpaka kumuua kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Shada Ibada (Pichani) kwa kumuhusisha na kundi l.akiharifu linalofahamika kwa jina la 'Waasi' ambalo kwa sasa limekuwa kero katika maeneo hayo. Mwandishi wa habari hizi ambaye alikuwa shuhuda wa tukio hilo amedai kuwa marehemu alikuwa akisakwa kwa muda mrefu kutokana na kujihusisha kwake na vitendo vya uharifu, kabla ya kuuawa marehemu alituhumiwa kuiba maeneo ya jirani ndipo alifukuzwa na wananchi wenye hasira na kumshushia kipigo kilichopelekea kifo chake. Tayari mwili wa marehemu umeshachukuliwa na polisi na kupelekwa hospitali kwa kuhifadhiwa, hivi karibuni kumezuka kwa vikundi vya vijana vinavyojhihusisha na uporaji, ubakaji na kuharibu amani ya watu, wakazi wa Tabata nao wamejikuta wakiishi kwa shida kufuatia kikundi cha 'Waasi' kuanzisha mtindo mchafu wa...

CHELSEA YAKABWA KOO NA WEST HAM UNITED, MOURINHO ALALAMA.

Picha
UMAARUFU wa Jose Mourinho na mafaniko aliyoyapata kutwaa mataji matatu ya Ligi Kuu ya Mabingwa Ulaya, vimetokana na mfumo wa uchezaji wa timu anazofundisha, kucheza kwa kujihami zaidi, maarufu kama kupaki basi. Lakini huwezi kuamini lakini Mourinho anaulaani vikali mfumo huo wa uchezaji, akiuita wa karne ya 19, ingawa yeye ameutumia miaka ya karibuni tu karne hii na kumjengea heshima na umaarufu mkubwa. Baada ya kulazimishwa sare ya 0-0 jana na West Ham United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England, kocha huyo wa Chelsea amemkandia kocha wa wapinzani wake, Sam Allardyce kucheza soka ya karne ya 19.

OWINO AUFYATA MKIA KWA LOGA, AREJESHWA KUIVAA OLJORO JKT

Picha
BEKI Joseph Owino amejishusha na kuomba radhi kwa kocha Zdravko Logarusic mbele ya wachezaji wenzake, juu ya tuhuma zake za utovu wa nidhamu na kujiona yuko juu ya wenzake- na bahati nzuri kwake amesamehewa na kurejeshwa kikosini. Habari kutoka ndani ya Simba SC zimesema kwamba, Owino aliandika barua ya kuomba radhi na baada ya hapo akaitwa kutakiwa kufanya hivyo mbele ya wachezaji wenzake pia, ili waridhie. Owino alipima kina cha maji kwa Logarusic, akagundua parefu hatimaye ameomba radhi na sasa amerejeshwa kundini Wachezaji wote wa Simba SC walipokea ombi la Owino kwa mikono miwili na kumkaribisha tena kundini, waendelee kupeperusha bendera nyekundu na nyeupe ya Mtaa wa Msimbazi. Lakini pamoja na kusamehewa, Owino atakatwa mshahara kwa siku zote ambazo hakuwa kwenye timu.

KAPOMBE KUREJEA SIMBA.

Picha
Uongozi wa klabu ya Simba umesema endapo beki, Shomary Kapombe, atashindwa kurejea AS Cannes inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Ufaransa, mchezaji huyo atalazimika kurejea katika klabu hiyo na hayatatokea kama yalivyojitokeza kwa aliyekuwa mshambuliaji wao, Emmanuel Okwi. Habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam jana zimeeleza kwamba Kapombe hataki kurejea Ufaransa licha ya madai yake dhidi ya klabu hiyo kutatuliwa. Akizungumza na jana, Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, alisema kwa sasa Kapombe ni mali ya wakala, Denis Kadito na kama kuna matatizo kati yake na wakala huyo wanatakiwa kukaa na kuzungumza ili kutimiza makubaliano waliyoingia kabla ya kujiunga na AS Cannes. Rage alisema wanaamini Kapombe bado ana nafasi ya kupata klabu barani Ulaya na atakapofanikiwa itakuwa ni faida kwa mchezaji husika na nchi pia.

YANGA YAIPISHA AZAM KILELENI, KIPRE TCHETCHE HATARI.

Picha
Mabingwa Yanga walishikwa kwa sare ya 0-0 ugenini mkoani Tanga dhidi ya Coastal Union na kushuhudia wakitema uongozi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya Azam FC kushinda 1-0 dhidi ya Rhino Rangers na kushika usukani wa ligi. Mbeya City ambao waliianza siku ya jana wakiwa na pointi 30 sawa na Azam, nao walidondosha pointi mbili jana kufuatia sare ya 1-1 ugenini Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini. Matokeo hayo yalimaanisha kwamba Azam sasa wako kileleni mwa msimamo wakiwa na pointi 33, moja juu ya Yanga walio katika nafasi ya pili, huku Mbeya City wakibaki katika nafasi yao ya tatu wakiwa na pointi 31.

MESSI HAUZWI, ASEMA BARTOMEU.

Picha
(Lionel Messi(kulia) akikabiliana na mchezaji wa klabu ya Malaga Juanmi) Mshambulizi matata wa Barcelona Lionel Messi hauzwi na kilabu hiyo inapanga kujadili mkataba mpya na raia huyo wa Argentina, amesema rais wa kilabu hiyo Josep Maria Bartomeu. Kuna uvumi kuwa Messi ambaye ni mshindi mara nne wa tuzo la Ballo d'Or, mwenye umri wa miaka 26, analengwa na kilabu ya Ufaransa ya Pris St-Germain. Lionel Messi ameshiriki pakubwa katika kusaidia Barcelona kufunga zaidi ya mabao 36 katika msimu huu na amekuwa katika kikosi cha ushindi mara 16 ati ya michezo 20 iliyochezwa.

MSANII WA BONGOFLEVA MATATANI KWA DAWA ZA KULEVYA TANGA.

Picha
MSANII wa muziki wa kjizazi kipya anayevuma sana kwenye mitandao ya kijamii kwa sasa Christopher Mhenga maarufu Mkola Man (Pichani) ameingia kwenye mzozo mwingine safari hii akihusishwa na matumizi ya dawa za kulevya na kupelekea kutengwa na baadhi ya marafiki Mambo Uwanjan i imeelezwa. Akizungumza na mtandao huu mara baada ya kuulizwa na mwandishi wa habari hizi kama kweli alifumwa akijidunga dawa hizo za kulevya, Mkola Man alikanusha vikali na kudai yeye atumii kabisa dawa hizo isipokuwa sigara tu. 'Mimi situmii kabisa dawa za kulevya nashangaa kusikia taarifa hizo kuwa natumia dawa, unajua tangia nimeanza kupata umaarufu kupitia wimbo wangu w a Kilevi changu  vyombo vya habari hasa mitandao ya kijamii vimekuwa vikiniandika tofauti', aliendelea kulalamika.

ARSENAL WAINGIA MKATABA MPYA MNONO NA PUMA

Picha
KLABU ya Arsenal imetangaza kuingia Mkataba wa muda mrefu wa udhamini wa vifaa vya michezo na kampuni ya Puma kuanzia Julai mwaka 2014. Pamoja na hayo hakuna kiwango cha fedha cha udhamini huo kilichothibitishwa Jumatatu, ingawa dili hilo linatajwa kama kubwa zaidi katika historia ya uhusiani wa Puma na Arsenal.

BIN SLUM AICHIMBA MKWARA YANGA, ASISITIZA KIPIGO KIKO PALEPALE MKWAKWANI.

Picha
MKURUGENZI wa Ufundi wa Coastal Union ya Tanga, Nassor Bin Slum amesema Yanga SC itakiona cha moto kwa timu yake keshokutwa katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Akizungumza na mtandao huu Bin Slum amesema kwamba vijana wake wapo vizuri kuelekea mchezo huo na hakuna shaka Yanga itaacha pointi zote tatu Uwanja wa Mkwakwani Jumatano. “Tunakubali msimu huu tumeshindwa kutimiza malengo yetu, siyo kwenye ubingwa tu, bali hata nafasi za nne za juu. Malengo yetu ya sasa ni kumaliza nafasi ya tano,”alisema Bin Slum.

BAINES AONGEZA MKATABA WA MIAKA MINNE EVERTON.

Picha
Mlinzi wa Everton Leighton Baines amerefusha muda wake wa kukaa katika klabu hiyo baada ya kutia saini mkataba mpya wa miaka minne, klabu hiyo ya Ligi ya Premia ilitangaza Jumatatu. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza alikuwa amesalia na miezi 17 kwenye mkataba wake Goodison Park na licha ya ripoti kwamba alikuwa akitafutwa na meneja wake wa zamani David Moyes akajiunge naye Manchester United, beki huyo wa kushoto wa umri wa miaka 29 aliambia kusalia Goodison Park. "Hatuwezi kueleza furaha tuliyo nayo kwamba klabu hii imepata miaka bora ya uchezaji wa Leighton Baines," meneja Roberto Martinez aliambia tovuti rasmi ya klabu hiyo (www.evertonfc.com). "Ni jambo la kutuongeza nguvu sana na la kuleta msisimko kuhusu siku za usoni. Leighton ametimiza tu miaka 29 majuzi na ana kiwango cha ukomavu na ujuzi wa soka katika pahala maalum uwanjani, na kuwepo kwake kwenye kikosi husikika.”

LOGA AIPONDA FOWADI SIMBA, AZIDI KUMUANDAMA MWOMBEKI.

Picha
 Baada ya kupata ushindi finyu katika mechi yake ya kwanza katika Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara, Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic 'Loga', amesema ligi hiyo ni ngumu na timu ndogo ndizo zimekuwa kikwazo kwa klabu kongwe za hapa nchini, lakini akaweka wazi kuwa washambuliaji wake bado hawajaelewa darasa lake. Simba juzi iliifunga Rhino Rangers ya mkoani Tabora bao 1-0 lililoiwezesha kufikisha pointi 27, hivyo kuendelea kukaa katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi hiyo inayoongozwa na wapinzani wao Yanga wakifuatiwa na Azam FC na Mbeya City.

YANGA WAIPANIA COASTAL UNION.

Picha
Na Elias John MABINGWA wa soka Tanzania bara Yanga, wameonyesha kuipania Coastal Union ya Tanga watakayokutana nayo keshokutwa jumatano kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga, Timu hizo ambazo zote zilikuwa nje ya nchi wakati zikijiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu bara zinakutana katika mchezo wa marudiano baada ya kutoka sare katika mechi yao ya kwanza iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Wakizungumza kwa nyakati tofauti wachezaji wa Yanga wamesema watacheza kufa na kupona ilikuondoka na pointi tatu katika mchezo huo,David Luhende ambaye kwa sasa anacheza kamakiungo wa pembeni ametamba ni lazima Yanga iibuke na ushindi katika mchezo huo ili kuendelea kuongoza ligi. 'Nimeipania sana Coastal, ni lazima tujitume ili tuambulie pointi tatu' alisema Luhende,Luhende ambaye katika mchezo wa kwanza uliofanyikja uwanja wa Taifa alisababisha penalti iliyozaa bao la kusawazisha la Coastal Union ambalo lilileta tafrani na kupelekea basi lililobeba wachezaji wa Coastal kupig...

WENGI WATAKUJA MAN UNITED BAADA YA MATA- MOYES

Picha
Meneja wa Manchester United, David Moyes, amesema jana kuwa kuvunja rekosi ya timu hiyo kumsajili Juan Mata kutoka Chelsea ndio mwanzo wa kuwasaini wachezaji wengi mwaka huu. United walikamilisha biashara ya kumleta Mata kwa pauni milioni 37.1 iliyogharimu zaidi kuliko pauni milioni 30.75 walizotoa kumsajili Dimitar Berbatov kutoka Tottenham Hotspur mwaka wa 2008. Moyes anatarajia Mata atasaidia kusitiri musimu ambao umeshuhudia mabingwa hao wa Ligi ya Premier wakifuata viongozi wa sasa Arsenal kwa alama 14 na kuondolewa kwenye vikombe viwili vya taifa hilo. United wanakisiwa kuanzisha majadiliano na nyota Wayne Rooney kutia kidole kandarasi mpya huku Moyes akidhibitisha juhudi za kuimarisha kikosi zitaendelea miezi ijayo.

OSCAR AIBEBA CHELSEA IKIIADHIBU STOKE.

Picha
Bao maridadi kutoka Oscar liliiongoza Chelsea kuwalaza Stoke City 1-0 katika raundi ya nne ya kombe la FA jana Jumapili. Kiungo huyo wa Brazil ambaye alichukua nafasi ya Juan Mata, aliyesajiliwa na Manchester United, kama kielelezo cha mashambulizi, alitia kimiani kutokana na mkwaju wa adhabu. Ubora wa bao lake nyota huyo lilidhihirisha sababu iliyomfanya meneja Jose Mourinho kuekeza imani naye na kumruhusu Mata kuondoka Stamford Bridge siku mbili zilizopita.

BALOTELLI ANG'ARA MILAN IKIIUA CAGLIARI

Picha
TIMU ya AC Milan imeifunga Cagliari mabao 2-1,shukrani kwao Mario Balotelli na Giampaolo Pazzini waliofunga mabao hayo.     Ilikuwa furaha kwa kocha moya Clarence Seedorf baada ya vijana wake kulipiku bao la mapema la Marco Sau na kuibuka na ushindi huo.

SIMBA YAITEKETEZA RHINO RANGERS, YAIPIGIA HESABU OLJORO JKT.

Picha
SIMBA SC imeanza vyema mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Ushindi huo, unaifanya Simba SC itimize pointi 27 baada ya kucheza mechi 14, ikibaki nafasi ya nne nyuma ya Yanga yenye pointi 31, Azam na Mbeya City pointi 30 kila moja. Hadi mapumziko, tayari Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na mshambuliaji Ramadhani Yahya Singano ‘Messi’ dakika ya 14. Messi alifunga bao hilo, baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Rhino na ndipo akaupitia mpira na kufumua shuti kali lililoipa ushindi huo Simba SC.

LIGI KUU BARA KIVUMBI LEO, YANGA VS ASHANTI, MTIBWA, AZAM HAPATOSHI CHAMANZI.

Picha
Baada ya kuwa katika mapumziko ya takribani miezi mitatu, Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo inaingia katika mzunguko wa pili wa lala salama, ambapo nyasi za viwanja vinne zitahitaji maji ili kuzima moto wa timu nane zitakazoshuka dimbani kukwaana. Viwanja vitakavyowaka moto leo ni Uwanja wa Taifa na Azam Complex vya jijini Dar es Salaam, Uwanja wa Mkwakwani,Tanga na Uwanja wa Kaitaba, Bukoba. Kwenye Uwanja wa Taifa, vinara na Mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Yanga watakabiliana na Ashanti United, wakati Azam wataikaribisha Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Azam Complex huku Coastal Union ikiwa mwenyeji wa JKT Oljoro itakayopimana nayo ubavu kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

CHELSEA YAMALIZANA NA SALAH.

Picha
Chelsea imemsajili mcheza kiungo wa timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah, kutoka kwa Basel ya Uswisi kwa kitita cha pauni milioni kumi na moja. Salah mwenye umri wa miaka 21, anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na pia kujadiliana kuhusu mshahara wake kabla ya kuhamia uwanja wa Stamford Bridge. Mahasimu wa Chelsea katika ligi kuu ya Premier, Liverpool walikuwa wameanzisha mazungumzo na klabu hiyo ya Basel, kutaka kumsajili mchezaji huyo.

OKWI KUIKOSA ASHANTI LEO, TFF YAIKAZIA YANGA.

Picha
YANGA SC wanahaha kumnasua mshambuliaji wao Mganda, Emmanuel Arnold Okwi aliyezuiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, hadi hapo ufafanuzi wa kesi yake na klabu ya Etoile de Sahel ya Tunisia utakapotolewa. TFF imesimamisha usajili wa Okwi Yanga wakati ikisubiri ufafanuzi kutoka Shirikisho la Soka la Kimataifa la (FIFA) juu ya kesi yake na Etoile. Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF iliyokutana Januari 22, mwaka huu kupitia masuala mbalimbali, imesimamisha usajili huo baada ya kubaini kuwa Okwi aliruhusiwa kuichezea SC Villa ya Uganda kwa kibali maalumu kutoka FIFA.

MOURINHO AKUBALI YAISHE KWA MATA, ADAI ILIKUWA KUMZUIA

Picha
KOCHA Jose Mourinho amesema Chelsea haikuwa na nguvu kumzuia Juan Mata kujiunga Manchester United. Mspanyola huyo amekwenda kufanyiwa vipimo Old Trafford ili rasmi awe mchezaji wa United atakapozufu. Dau la Pauni Milioni 37 tayari limesainiwa na klabu zote na vipengele binafsi vya Mkataba vimefikiwa na mchezaji huyo.

MAKALA: DINO MANYUTI, NYOTA MPYA BONGOFLEVA ANAYETAMBA NA TAM TAM.

Picha
Na Exipedito Mataruma Kizazi kipya ndani ya bongofleva, apania na wimbo wake Tam tamNi kijana mdogo anayetokea kukonga nyoyo za mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kwa sasa na wimbo wake wa Tam tam ambao umeanza kupata wafuasi wengi. Kutamba kwa wimbo wake huo kunaweza kumfanya afikie dhamila yake ya kujulikana na kuweza kupata mafanikio kama ilivyo kwa nyota wengine wa muziki huo wa kizazi kipya. Bila shaka mbuyu ulianza kama mchicha, hata masupa staa wa sasa kama Naseeb Abdul maarufu Diamond Plutinum, Ommy Dimpoz, Rich Mavoko, Ay na wengineo hawakuanza kujulikana ghafra, walitumia muda wao mpaka kufahamika na sasa wanafaidi matunda ya muziki. Abdalah Ramadhani Manyuti a.k.a 'D Sina shaka' (Pichani) ameanza kupata unafuu baada ya kusota kwa muda mrefu kwenye muziki huo bila mafanikio yoyote, Kijana huyo anaweza kufikia nyendo za wakali wengine wa muziki huo.

CHELSEA YAKUBALI KUMUUZA JUAN MATA KWA MAHASIMU WAO.

Picha
Ofa ya Manchester United ya £37 milioni ya kumnunua kiungo wa kati Juan Mata imekubaliwa na wapinzani wao katika Ligi ya Premia Chelsea, gazeti la Uingereza la Daily Telegraph liliripoti Jumatano. Gazeti hilo lilisema Mata alikubaliana na klabu hiyo kuhusu matakwa ya kibinafsi na kwamba angefanyiwa uchunguzi wa kimatibabu Alhamisi. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania amekuwa akihusishwa na kuhama Stamford Bridge baada ya kushindwa kupata nafasi ya kuanza chini ya meneja Jose Mourinho. Mchezaji huyo wa miaka 25 amekuwa hapati muda wa kucheza, huku Mourinho akipendelea Wabrazil Oscar na Willian na Mbelgiji Eden Hazard. United chini ya meneja David Moyes inatafuta nguvu mpya kuimarisha kikosi baada ya mwanzo mbaya kwenye msimu kuacha klabu hiyo ikiwa nambari saba kwenye Ligi ya Premia na alama 14 nyuma ya viongozi Arsenal.

TFF YAICHINJA YANGA, YASITISHA USAJILI WA OKWI, YAPANGUA RATIBA LIGI KUU.

Picha
Na Boniface Wambura, Ilala SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesimamisha usajili wa mshambuliaji Emmanuel Okwi kutoka Uganda katika timu ya Yanga wakati likisubiri ufafanuzi kutoka Shirikisho la Soka la Kimataifa la (FIFA). Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF iliyokutana jana (Januari 22 mwaka huu) kupitia masuala mbalimbali, imesimamisha usajili huo baada ya kubaini kuwa Okwi aliruhusiwa kuichezea SC Villa ya Uganda kwa kibali maalumu kutoka FIFA.  Okwi ambaye aliingia mgogoro na klabu yake ya Etoile du Sahel ya Tunisia aliruhusiwa na FIFA kuchezea SC Villa kwa kibali maalumu (provisional permit) cha miezi sita ili kulinda kiwango chake wakati suala lake dhidi ya Etoile du Sahel likishughulikiwa na shirikisho hilo la kimataifa.

BODI YA LIGI YAIKABA KOO YANGA KUHUSU AZAMTV

Picha
Uongozi wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), umesema Yanga itake isitake AzamTV itarusha mechi zote na kama hawataki ni bora wakajitoa kwenye Ligi. Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Ahmad Yahaya akijibu azimio lililofikiwa na viongozi na wanachama wa Yanga wa kugomea AzamTV kuonyesha mechi zake. Yahaya alisema Yanga hawana haki ya Televisheni za Ligi Kuu mwenye haki hizo ni Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

MAN UNITED SASA NYOKA WA KIBISA.

Picha
David Moyes ameendelea kuwanyima raha mashabiki wa Manchester United, baada ya usiku wa jana timu hiyo kutolewa katika Nusu Fainali ya Kombe la Ligi, kwa penalti 2-1 kufuatia sare ya jumla ya 3-3 Uwanja wa Old Trafford, Manchester, England. Sunderland ilishinda 2-1 katika mchezo wa kwanza nyumbani na leo ikalala 2-1 baada ya dakika 120. Evans alianza  kuifungia United dakika ya 37 na bao hilo likadumu hadi dakika 90 ndipo zikaongezwa dakika 30 na Bardsley akaisawazishia Sunderland dakika ya 119.

EZEKIEL KAMWAGA KATIBU MKUU MPYA SIMBA, MUHAJI AFISA HABARI.

Picha
MWENYEKITI wa Simba SC, Alhaj Ismail Rage anatarajiwa kumtaja Ezekiel Kamwaga kuwa Katibu mpya wa klabu hiyo, nafasi iliyoachwa wazi na Evodius Mtawala aliyejiuzulu baada ya kuteuliwa Shirikisho la SOka la SOka Tanzania (TFF). Aidha, mbunge huyo wa Tabora Mjini CCM, atamtaja pia Mwandishi mwandamizi wa magazeti ya Bingwa na Dimba, Asha Muhaji kuwa Ofisa Habari mpya wa klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi, nafasi ambayo inaachwa wazi na Kamwaga anayepanda cheo. Habari kutoka ndani ya Simba SC, zimesema kwamba Rage atakuwa na Mkutano na Waandishi

ADEBAYOR AZIDI KUNG' ARA LIGI KUU ENGLAND

Picha
Emmanuel Adebayor alifunga mawili na kusaidia Tottenham kuwatoa wenyeji Swansea manyoa 3-1 kuendeleza matokeo bora chini ya utawala mpya wa meneja Tim Sherwood. Mshambuliaji huyo wa Togo alisaidia klabu chake kuandikisha alama sawa na Liverpool walioko nafasi ya nne huku Sherwood akisherehekea ushindi wa tano na sare moja katika ligi ya Premier baada ya kumrithi Andre Villas-Boas. Swansea walisalia alama tatu mbele ya eneo la hatari baada ya kuenda mechi nane bila ushindi. Adebayor alipata la ufunguzi kati ya kipindi cha kwanza pale alipozamisha krosi safi kutoka kwake Christian Eriksen.

HILI NDIO BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI.

Picha
Rais Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri ambapo amewatupa nje mawaziri watano, kuwaingiza 10 wapya, kuwapandisha manaibu wanne kuwa mawaziri kamili na kuwahamisha wengine wanane kutoka wizara zao kwenda nyingine. Miongoni mwa walioachwa katika mabadiliko yaliyotangazwa jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue jana, ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk Terezya Huvisa ambaye nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa Naibu Waziri wa Maji, Dk Binilith Mahenge. Wengine walioachwa na wizara zao kwenye mabano ni Manaibu Waziri, Goodlucky Ole Medeye (Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi), Gregory Teu (Viwanda na Biashara), Benedict Ole Nangoro (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi) na Philipo Mulugo (Elimu na Mafunzo ya Ufundi).

DIDA AMFUNIKA KASEJA UTURUKI, MHOLANZI AIMWAGIA SIFA BEKI YANGA.

Picha
Na Baraka Kizuguto, Antalya BAADA ya sare ya 0-0 juzi na KS Flamurtari inayoshiriki Ligi Kuu ya Albania katika viwanja vya Side Stars Complex Manavgat, Antalya, Kocha Mkuu wa Yanga SC, Mholanzi Hans van der Pluijm ameusifu ukuta wa timu yake ni imara. Alisema vijana wake wamecheza vizuri mechi ya juzi na kwa ujumla timu zote ziliweza kucheza kwa nafasi, lakini kwa umakini wa walinzi wa timu zote ndio maana milango ilikua migumu kufunguka. “KS Flamurtari ni timu nzuri, awali hawakutegemea kama watapata ushindani mkali kutoka kwetu, lakini kadri mchezo ulivyokua ukiendelea walishangaa kuona tuna kikosi safi kilichokamilika,”.

HATIMAYE ETO'O AKATA NGEBE ZA MOYES, AZIDI KUWALIZA MAN U.

Picha
MCAMEROON Samuel Eto'o amelichangamsha Jiji la London jana baada ya kufunga mabao yote matatu katika ushindi wa 3-1 wa Chelsea dhidi ya Manchester United, Uwanja wa Stamford Bridge. Eto'o alifunga mabao mawili kipindi cha kwanza dakika ya 17 na 45 na baadaye dakika ya nne tangu kuanza kipindi cha pili akakamilisha hattrick yake kabla ya kumpisha Fernando Torres dakika ya 79. Javier Hernandez 'Chicharito' aliyetokea benchi dakika ya 56 kuchukua nafasi ya Ashley Young aliwafungia Mashetani Wekundu bao la kufutia machozi dakika ya 78.

SHOMARI KAPOMBE HATIHATI KUTUA YANGA AU AZAM.

Picha
Beki wa zamani wa Simba ya jijini Dar es Salaam, Shomary Kapombe, amesema yeye sasa ni mchezaji huru na yuko tayari kufanya mazungumzo na klabu yoyote ya ndani na nje ya nchi ambayo itahitaji huduma yake. Kapombe ambaye kwa sasa yuko hapa nchini, alikuwa akilelewa kisoka Ufaransa katika Klabu ya AS Cannes akiichezea kwa mkopo kwa lengo la kutumia nafasi hiyo kupata uzoefu wa ligi ya nchi hiyo kabla ya kutafutiwa soko. Simba ilimtoa beki huyo na kumpeleka Ufaransa kupitia wakala wa mchezaji huyo. Akizungumza juzi jijini, Kapombe, alisema baada ya Klabu ya AS Cannes kusitisha malipo yake ya mshahara na posho, aliamua kuikacha na kutorejea huko kuendelea na timu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la nne.

VAN PERSIE AMTABIRIA MAKUBWA MOYES.

Picha
Robin van Persie amesema ana imani kwamba meneja wa Manchester United anayekabiliwa na shinikizo David Moyes atafana Old Trafford. Moyes amekumbana na mwanzo mbaya wa ufanyakazi wake United kwani timu hiyo imehangaika katika juhudi zake za kutetea taji la Ligi ya Premia na pia ilibanduliwa kutoka kwa Kombe la FA raundi ya tatu. United wako alama 11 nyuma ya viongozi Arsenal na wanakabiliwa na mlima katika juhudi zao za kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao. Kumekuwa na uvumi kwamba Moyes ameshindwa kupata imani kutoka kwa baadhi ya wachezaji wa United. Na mahangaiko ya klabu hiyo katika juhudi zake za kudumisha viwango vya miaka ya Alex yamepelekea kushuka kwa thamani ya hisa za klabu katika Soko la Hisa la New York.

RONALDO KUWANUNULIA GARI JIPYAAAA MADAKTARI REAL MADRID...NI FURAHA YA BALLON D'OR

Picha
NI kazi ngumu kuwa mchua misuli wa Cristiano Ronaldo, lakini wakati mwingine inalipa.    Mchezaji huyo ambaye hivi karibuni ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia, FIFA Ballon d’Or amewaahidi madaktari wa Madrid kuwanunulia gari mpya baada ya kushinda tuzo hiyo wiki hii.   Katika mahojiano ya hivi karibuni na  Sportsmail , kocha wa Real Madrid, Paul Clement amezungumzia mambo ambayo Ronaldo atayafanya atakaporejea kutoka kwenye mechi za katikati ya wiki za Ligi ya Mabingwa.

WATATU COASTAL UNION WAPATA ULAJI OMAN.

Picha
WACHEZAJI watatu wa timu ya soka ya Coastal Union ya Tanga, beki Juma Nyosso, kiungo Jerry Santo na mshambuliaji Danny Lyanga wanatakiwa na klabu ya Al Musannaa ya Ligi Kuu ya Oman, imefahamika. Habari ambazo tumezipata kutoka Oman zimesema kwamba klabu hiyo imekwishakutana na Jerry Santo kulia akiwa na Salum Esry jana kabla ya chakula cha usiku. Hata hivyo, habari zaidi zinasema makubaliano hayajafikiwa kutokana na Coastal kusema Musannaa imetoa ofa ndogo ya kuwanunua nyota wake hao. Inaelezwa, kiungo Mkenya, Jerry Santo anatakiwa pia klabu ya Fanja, ambayo hadi sasa ina mgeni mmoja tu kikosini mwake, Cisse wa Senegal. Jana tena Aurora alikuwa ana kikao na uongozi wa Musannaa hata akashindwa kuhudhuria mwaliko wa chakula cha usiku, ambao Coastal walipewa na mwanachama wa timu hiyo anayeishi hapa, Salum Esry.

TUPO TAYARI KWA LIGI KUU-LOGARUSIC

Picha
Kocha wa klabu ya Simba Zdravko Logarusic 'Loga' amesema kuwa hana shaka na kikosi chake na kwa sasa timu yake ipo tayari kwa mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara. Akizungumza jana, Loga, alisema kuwa michezo ya kombe la mapinduzi imewaimarisha zaidi wachezaji wake na kwa sasa wanasubiri mzunguko wa pili wa ligi kuu. Alisema kuwa wachezaji watakaopata nafasi kwenye mzunguko wa pili wa ligi ku ni wale watakaoonyesha uwezo. "Mechi tulizocheza Zanzibar zimetumarisha zaidi ni maandalizi mazuri kwa ajili ya ligi..., sina shaka na timu yangu kwa sasa tupo tayari kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi kuu," alisema Loga.

YANGA KUTUPA KARATA NYINGINE LEO UTURUKI, KUCHEZA NA TIMU YA LIGI KUU.

Picha
Mabingwa wa soka nchini, Yanga wanaendelea na mandalizi yao kwa ajili ya ligi kuu na mashindano ya kimataifa na leo wanacheza mchezo wa tatu wa kirafiki dhidi ya KS Flamurtari Vlore inayoshiriki ligi kuu nchini  Albania. Yanga ipo nchini Uturuki ilipokwenda kuweka kambi na itacheza na timu hiyo ambayo nayo ipo nchini humo kwa ziara ya mafunzo. Akizungumza kwa njia ya simu, Afisa Habari wa klabu hiyo, Baraka Kizuguto, alisema kuwa mchezo huo wa leo ni sehemu ya mafunzo yao na kocha mpya wa timu hiyo, Johanes Franciscus 'Hans' van der Pluijm anataka kutumia michezo ya kirafiki nchini humo kukifahamu vizuri kikosi chake.

MISRI YASHANGAZA VIWANGO VYA SOKA DUNIANI.

Picha
Misri imepiga hatua kubwa zaidi miongoni mwa timu za Afrika katika orodha ya kwanza mwaka 2014 ya FIFA . Imepanda alama kumi juu hadi katika nafasi ya 31 duniani. Inamaanisha kuwa Misri ni ya nne katika ubora barani Afrika ikiwa juu ya taifa ya Nigeria walioshuka hadi nafasi ya saba.

LOWASSA AIGAWA CCM VIPANDE VIPANDE.

Picha
Makundi ya Urais wa 2015 yanaendelea kuivuruga CCM baada ya Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Singida, Mgana Msindai kuibuka na kusema atamburuta mahakamani Mwenyekiti mwenzake wa Mkoa wa Geita, Joseph Kasheku ‘Msukuma’ asipomwomba radhi kwa kumchafua kwa kumwita mpuuzi. Hata hivyo, Kasheku amesema Msindai anaweza kwenda mahakamani huku akisisitiza kwamba hawezi kumwomba radhi kwa kuwa anaamini kwamba alichofanya ni kinyume cha taratibu za chama na vikao. Juzi, Kasheku alimponda Msindai mbele ya waandishi wa habari kwa kitendo chake cha kusema kuwa wenyeviti wa CCM wa mikoa yote ya Tanzania wanamuunga mkono, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa katika safari yake ya urais wa 2015 wakati wa sherehe ya mwaka mpya huko Monduli, Arusha.

LOGARUSIC APANIA KUIVURUGA YANGA YA 'KIBABU'

Picha
Kocha wa Simba, Zdravco Logarusic amesema hawezi kupoteza muda kwa kupigana vijembe na kocha wa Yanga, Mdachi Hans Van Der Pluijim, atamshushia heshima kwa kuhakikisha anatwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu. Akizungumza na Mtandao huu, Logarusic  alisema ujio wa Pluijm haumpi tabu, kwa vile mechi aliyopoteza wakati akiifundisha Ashanti Gold ya Ghana haikuwa ya mashindano rasmi bali  maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu ya nchini humo. “Nataka ufahamu kwanza imepita miaka mitatu tangu tulipokutana na mimi kupoteza mchezo, ni muda mrefu sana umepita  siyo jana.

COASTAL UNION WABEBA NDOO OMAN BAADA YA MIAKA 26.

Picha
 MARA ya mwisho Coastal Union ya Tanga kushinda taji ilikuwa ni mwaka 1988 walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wakati huo ikiitwa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara. Tangu wamekabidhiwa Kombe la ubingwa wa Bara, Coastal hawajawahi kukabidhiwa taji lingine kwa sababu hawajashinda mashindano yoyote mengine baada ya hapo. Lakini jana, ikiwa ni miaka 26 baadaye, timu hiyo ilipewa taji, baada ya kukabidhiwa Ngao ya Urafiki na klabu ya Fanja ya Oman, kutokana na kuzuru nchini hapo kucheza mechi ya kirafiki na klabu hiyo kigogo.

MESSI HATARI APIGA MBILI KOMBE LA MFALME, NEYMAR MAJANGA.

Picha
 MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Neymar ameumia kifundo cha mguu akiichezea timu yake mechi ya Copa del Rey ikishinda 2-0 jana dhidi ya Getafe katika mechi ya Kombe la Mfalme. Sasa Mbrazil huyo anaweza kuukosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester City mwezi ujao. Lionel Messi alifunga mabao yote katika mechi hiyo ya marudiano ya 16 Bora na kufanya ushindi wa jumla wa 6-0.

MAAJABU: MOYES KUWANIA MENEJA BORA WA LIGI YA PREMIA

Picha
Meneja wa Manchester United David Moyes, ambaye amepokezwa vichapo mara tatu mfululizo 2014, ameorodheshwa kupigania tuzo ya Meneja Bora wa Mwezi wa Desemba katika Ligi ya Premia. Timu ya Moyes imekumbana na mwanzo mbaya wa Mwaka Mpya lakini ilikuwa imefanikiwa kushinda mara nne, kutoka sare mara moja na kushindwa mara mbili pekee kwenye mechi saba za ligi mwishoni mwa 2013. Raia huyo wa Scotland ameorodheshwa pamoja na meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini, ambaye hakushindwa Desemba, Jose Mourinho na Roberto Martinez wa Everton. Chelsea walishinda mara tano kwenye mechi saba, wakatoka sare moja na kushindwa mara moja huku Martinez, aliyerithi Moyes Everton, akiongoza vijana wake kushinda mara nne katika mechi sita, kutoka sare moja na kushindwa moja.

MZUNGU WA SIMBA AKERWA NA JEURI YA FEDHA YA YANGA, APONDA ZIARA YA UTURUKI.

Picha
Baada ya Yanga kwenda kuweka kambi Uturuki, Kocha wa Simba, Zradvok Logarusic ameibeza safari hiyo na kuhahidi kuendeleza kutoa kipigo kwa mabingwa hao. “Siku zilizobaki ni chache sana, kuwapeleka wachezaji kule ni mbali na hali ya hewa ya huku na kule nadhani ni tofauti labda kwa vile wana fedha. “Mtu ukishakuwa na fedha unaenda sehemu yoyote duniani, unafanya chochote, Yanga wanahela mimi sijui wamezipata wapi, lakini wanatakiwa kuangalia pia na wakati, mimi sihitaji kwenda sehemu yoyote nje ya Dar es Salaam. “Nataka kurudi Dar mara moja baada ya mashindano haya., nimechoka., Wwachezaji wangu nao wamechoka, sihtaji kuendelea kubaki hapa hata kwa siku moja zaidi., Nnimeshawaambia viongozi kambi itakuwa Dar.

AZAM YAVULIWA RASMI UBINGWA WA MAPINDUZI.

Picha
Mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi, Azam FC jana walivuliwa ubingwa baada ya kukubali kipigo cha magoli 3-2 kutoka kwa KCC ya Uganda kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza uliochezwa kwenye uwanja wa Amaan kisiwani hapa. Azam ndio waliokuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa nyota wa mchezo huo, ‘yoso’ Joseph Kimwaga katika dakika ya 16 akimalizia kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na beki wa pembeni Erasto Nyoni. Azam waliendelea kuliandama goli la KCC na katika dakika ya 32 kimwaga tena aliipatia Azam goli la pili akimalizia kwa mguu wa kulia pasi ya ‘kupenyeza’ iliyopigwa na Kipre Tchetche baada ya raia huyo wa Ivory Coast kuwachambua mabeki wa KCC kabla ya kutoa pasi hiyo kwa mfungaji.

JESHI LA YANGA NOMA UTURUKI.

Picha
Mabingwa wa soka nchini, Yanga, jana walianza rasmi mazoezi wakiwa nchini Uturuki walipokwenda kuweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu na mashindano ya kimataifa. Kikosi cha Yanga jana asubuhi kilifanya mazoezi kwenye uwanja uliopo ndani ya Hoteli waliyofikia ya Sueno Beach mjini Antalya. Akizungumza kwa njia ya simu, Kocha wa timu hiyo, Charles Mkwasa aliyeambatana na timu hiyo alisema kuwa programu yake rasmi ya mazoezi anaianza leo Jumamosi.

SIMBA YATISHA ZANZIBAR, YATINGA FAINALI KWA KISHINDO.

Picha
SIMBA SC wamefuzu kuingia Fainali ya Kombe la Mapinduzi, baada ya jana usiku kuilaza mabao 2-0 URA ya Uganda kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Shujaa wa Simba SC jana alikuwa ni kiungo mwenye kipaji, Amri Ramadhani Kiemba aliyesababisha bao la kwanza na kufunga mwenyewe la pili. URA ilipata pigo mapema dakika ya 32 baada ya mshambuliaji wake hatari, Owen Kasule kutolewa nje kwa nyekundu ya moja kwa moja kwa kumchezea rafu winga msumbufu wa Simba SC, Ramadhani Singano ‘Messi’.

MAJANGA YAZIDI KUIKUMBA MAN UNITED, VAN PERSIE BASI TENA.

Picha
KLABU ya Manchester United inahofia Robin van Persie anaweza kuendelea kuwa nje kwa wiki sita zaidi baada ya kuumia paja sehemu ile ile aliyowahi kuumia alipokuwa Arsenal. David Moyes anayemuhitaji sana mshambuliaji huyo wake hatari arejee uwanjani kutokana mwenendo mbaya wa timu hivi sasa, jana Ijumaa amethibitisha kwamba Wayne Rooney pia anaweza kukosa mechi ya leo dhidi ya Swansea. Lakini mtu anayemuumiza kichwa aswa Moyes ni Van Persie, kocha huyo amesema kwamba hawezi kutaja tarehe ya kurejea uwanjani kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30, hata baada ya kumpeleka Uholanzi akafanyiwe kazi na kocha wa viungo wa PSV Eindhoven.

MOYES SASA KUSAJILI NYOTA WAPYA.

Picha
David Moyes, ambaye anazidi kuzingirwa na matatizo chungu mzima kwenye utawala wake mchanga Mancheter United amekiri anahitaji kununua nguvu mpya kwa dharura katika soko la Januari. Lakini mwalimu huyo pia alikubali kuwa hilo linaweza kutibuka kutokana na hali wasi wasi ya kifedha katika mabingwa hao wa Ligi ya Premier ya Uingereza. Moyes alikuwa anazungumuza muda mchache baada ya kushuhudia vijana wake wakingatuliwa kutoka Kombe la FA na Swansea waliowanyoa 2-1 nyumbani kwao Old Trafford Jumapili. “Nitajaribu lakini ninashauku kuwa naweza leta wachezaji wapya hapa Januari. Kuna dharura ya kusajili viungo wapya lakini swali ni, watapatikana? “Hakuna haja ya kusema mengi kwani wachezaji tunaotamani huenda wasipatikane Januari,” Moyes alisema baada ya United kushindwa kwa mara ya nne nyumbani ndani ya mechi sita.