VAN PERSIE AMTABIRIA MAKUBWA MOYES.

Robin van Persie amesema ana imani kwamba meneja wa Manchester United anayekabiliwa na shinikizo David Moyes atafana Old Trafford.

Moyes amekumbana na mwanzo mbaya wa ufanyakazi wake United kwani timu hiyo imehangaika katika juhudi zake za kutetea taji la Ligi ya Premia na pia ilibanduliwa kutoka kwa Kombe la FA raundi ya tatu.

United wako alama 11 nyuma ya viongozi Arsenal na wanakabiliwa na mlima katika juhudi zao za kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao.

Kumekuwa na uvumi kwamba Moyes ameshindwa kupata imani kutoka kwa baadhi ya wachezaji wa United.

Na mahangaiko ya klabu hiyo katika juhudi zake za kudumisha viwango vya miaka ya Alex yamepelekea kushuka kwa thamani ya hisa za klabu katika Soko la Hisa la New York.


Lakini straika wa United Van Persie, ambaye amekosa sehemu kubwa ya msimu huu kutokana na jeraha la paja, ana imani kwamba Moyes atafanikiwa akipewa muda.

“Ninafikiri kwamba anahitaji muda sawa na watu wengine wote, hasa ukiwa mgeni katika klabu kubwa,” Van Persie aliambia gazeti la Guardian.

"Na kwa kweli, sidhani kwamba watu hawaelewi kwamba wanahitaji kumpa muda zaidi, na naongea kuhusu mashabiki na hata sisi.

“Atapata muda huo na kila mmoja anajua kwamba tutabadilisha mambo karibuni.

“Tulipoteza alama nyingi msimu huu, nyingi sana, lakini ikiwa unataka kupigania mataji yote, ni lazima ucheze vyema na ushinde mechi nyingi – lakini tunafanya kila tuwezalo kubadilisha hilo.

"Meneja ndiye kiongozi wetu katika hilo na anajaribu kadiri awezavyo na ninafikiri atabadilisha mambo.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA